*************************
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
April 7
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambayo inatarajiwa kufanyika katika chuo cha Uongozi cha mwalimu Nyerere kilichoko Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Pwani ,Mkuu wa mkoa huo Abubakari Kunenge amesema sambamba na kumbukizi hiyo ya baba wa Taifa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Pwani kimeandaa mdahalo .
Mdahalo huo una lengo la kutafakuri maisha ya mwalimu Nyerere ambao utafanyika April 9 mwaka huu katika chuo hicho.
Kunenge amebainisha,kila april 13 huwa kumbukizi ya kuzaliwa safari hii ,kumbukizi hii itatimiza miaka 100 ya mwl.Nyerere.
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere alizaliwa April 13 , mwaka 1922 kijijini Butiama mkoa wa Mara, na amefariki dunia mwezi October mwaka 1999.