BAADHI ya Wajumbe wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika wakiwa katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar uliofunguliwa leo rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika leo unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika leo unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
BAADHI ya Wajumbe wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi rasmi wa Mkutano huo unaofanyika Hotelini hapo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Zubeir Ali Maulid na Spika wa Bunge la Kenya pia Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji Chama cha Mabunge Justin Maturi (katikati) wakiongozwa na Mpambe Mwinyi Haji Abu(mwenye Siwa) wakati leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiingia katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kufungua Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Spika wa Mabunge wa Nchi mbali mbali wakisimama wakati Wimbo wa Taifa wa Ukipigwa katika ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai (kulia) Spika wa Bunge la Kenya pia Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji Chama cha Mabunge Justin Moturi (katikati) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Zubeir Ali Maulid (wa pili kushoto) na Spika wa Bunge la Uganda Rebecca Alitwala Kadaga wakisimama wakati Wimbo wa Taifa wa Ukipigwa katika ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Picha na Ikulu
………………
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kwamba teknolojia ya habari na mawasiliano ina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko ya maendeleo katika Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola.
Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo katika ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Chama Cha Mabunge cha Jumuiya ya Madola (CPA) Kanda ya Afrika unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinatul Bahr, iliyopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Rais Dk. Shein alisema kwamba iwapo teknolojia ya habari na mawasiliano itatumika ipasavyo hasa katika kuimarisha kanzi data mbali mbali hatua hiyo itarahisisha suala zima la kufanya maamuzi kwa wakati na kuweza kufikia malengo yaliokusudiwa.
Aliongeza kuwa uendeshaji wa Bunge kwa kutumia njia za kisasa kunawaweka karibu zaidi Wabunge na wananchi, jambo ambalo linatoa fursa pana zaidi kwa wananchi ya ya kutoa maoni yao na hoja mbali mbali za maendeleo zinazogusa maisha yao ya kila siku.
Alieleza kuwa Bunge Mtandao ni nyenzo nzima ya kupunguza harama za mambo mbali mbali kama vile usafiri sambamba na kuokoa muda.