Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akizindua baadhi ya vitabu wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akikagua baadhi ya vitabu wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akizungumza wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu (Elimu) Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu, OR TAMISEMI (Elimu) Mhe.Gerald Mweli akizungumza wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Lugoba, Kuruthumu Moshi akisoma kitabu cha nukta nundu wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akiwa na baadhi ya viongozi wa waizara wakipata picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda(katikati) akiwa na baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo wakionesha baadhi ya vitabu vilivyozinduliwa wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akizindua moja ya bajaji ambayo itatumika kwa walimu wenye mahitaji maalumu wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu (Elimu) Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo akizindua moja ya bajaji ambayo itatumika kwa walimu wenye mahitaji maalumu wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu uliofanyika leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilipokea kiasi cha bilioni 64 kwa ajili ya mradi wa maendeleo kwa ustawi na mapambano dhidi ya UVIKO 19 hivyo kupitia mradi wa mpango huo, Wizara ilipokea jumla ya Shilingi 707,000,000/- kwa ajili ya kuchapa vitabu vya kiada kwa matumizi ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Ameyasema hayo leo Aprili 5,2022 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda wakati wa uzinduzi wa kazi ya Kusambaza vitabu vya Breli na Maandishi yaliyokuzwa pamoja na ugawaji wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa vyuo vikuu.
“Fedha hii imeweza kuchapa jumla ya nakala 9,100 ya vitabu vya Braille vyenye jumla ya juzuu 32,140 pamoja na vitabu vya michoro mguso vyenye jumla ya juzuu 20,400”. Amesema Waziri Mkenda.
Aidha Waziri Mkenda amesema Wizara imeweza kuchapa vitabu vya kiada vya Maandishi yalikuzwa nakala 60,283 kwa ajili ya wanafunzi wenye uoni hafifu ambavyo vimechapwa katika uwiano wa vitabu vitatu kwa mwanafunzi mmoja (3:1).
Amesema Vitabu hivyo vitawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya uoni kujifunza kama ilivyo kwa wanafunzi wengine na kupata stadi na mahiri mbalimbali zitakazowawezesha kumudu changamoto mbalimbali katika tendo la kujifunza.
Hata hivyo amesema Serikali imekuwa na mahusiano mazuri na wadau mbalimbali wa maendeleo, na kupitia mahusiano hayo imepata msaada wa kuandaa na kuchapa vitabu kutoka shirika lililopo nchini Korea Kusini liitwalo “Siloam Center for the Blind” lenye ofisi zake ndogo mkoani Kilimanjaro.
“Shirika hili limeweza kuchapa vitabu vya kiada vya Breli kwa sekondari kidato cha 1-6 nakala 4,000 za masomo ya English, History, Geography, Fasihi na Lugha na Sarufi kwa uwiano wa vitabu vitatu kwa mwanafunzi mmoja (3:1)”. Amesema
Waziri mkenda amesema Serikali imenunua Tablets 175 kwa ajili ya kupakia kamusi ya Lugha ya Alama ya Tanzania kwa ajili ya wanafunzi viziwi na Audiometer 39 kwa ajili ya kupima kiwango cha usikivu kwa wanafunzi viziwi.
Ameeleza kuwa Vitabu hivyo vinakusudiwa kusambazwa kwa wanafunzi 3,677 katika shule 764 za wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu Tanzania Bara na Zanzibar pia vifaa maalum na saidizi vitagawiwa kwa wanafunzi 364 wenye ulemavu wa viungo, wasioona na wenye uziwi wanaosoma katika vyuo vikuu 11.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba amesema vitabu hivyo vitasambazwa katika halmashauri zote Tanzania bara na visiwani kwenye shule zote zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa uwiano wa vitabu viitatu kwa mwanafunzi mmoja na vya maandishi yaliyokuzwa vinasambazwa kwa uwiano wa 3:1.
Uwiano wa 3:1 ndo stahiki kwa matumizi ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Shule zitakazonufaika zenye wanafunzi wenye uoni hafifu ni 697 na shule zenye wanafunzi wasioona ni 68″. Amesema
Amesema vitabu walivyopokea kutoka shirika la Siloam Center for Blind la nchini Korea ni vitabu vya kiada ambavyo viliandikwa na TET na ubadilishwaji wa vitabu hivyo umefanywa kwa kutumia wataalamu wa TET na wale wa nchini Korea na uchapishwaji umefanyika nchini Korea.
Pamoja na hayo ameishukuru Serikali kwa kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wote bila kujali hali zao za kimaumbile.