Naibu Waziri wa Ujenzi, Eng. Godfrey Kasekenya, akijibu swali katika mkutano wa saba wa Bunge unaoendelea, jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete, akijibu swali katika mkutano wa saba wa Bunge unaoendelea, jijini Dodoma
************************
PICHA NA WUU
Akijibu swali Bungeni leo lililoulizwa na Mbunge wa Nyamagana, Mhe. Stanslaus Mabula, Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Kasekenya amesisitiza kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa barabara hiyo iko katika hatua za mwisho na inatarajiwa kukamilika baadae mwezi huu.
Amesema baada ya usanifu wa kina kukamilika na gharama za ukarabati kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ukarabati utakaohusisha upanuzi wa barabara hiyo.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Atupele Mwakibete, amesema ili kuondokana na changamoto ya upungufu wa mabehewa, Shirika la Reli Tanzania (TRC), inakarabati mabehewa 37 ili kuimarisha huduma ya usafiri wa treni mkoani Kigoma.
Mhe. Mwakibete alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Kilumbe Ng’enda, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuboresha usafiri wa Reli ya Kigoma – Dar es Salaam ambao umekuwa ukifanya safari mbili kwa wiki badala ya safari moja kila siku kama ilivyokuwa awali.
Naibu Waziri Mwakibete, amelihakikishia Bunge kuwa Serikali inaendelea na zoezi la ukarabati na ununuzi wa mabehewa ya abiria na baada ya utekelezaji wa kazi hizo, idadi ya safari za treni kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma zitaongezeka kutoka safari mbili hadi nne kwa wiki.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi