NJOMBE
Ikiwa siku nne zimesalia kuanza kutekelezwa kwa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki nchini,wafanyabiashara wakubwa wa mifuko hiyo mjini Njombe wameiomba serikali kuwaongezea muda wa kutekeleza katazo hilo ili kuwaepusha na hasara kwani bado wanahazina kubwa gharani.
Wakizungumzia mwamko wa wateja katika kununua vifungashio vipya baadhi ya wafanyabiashara wa mifuko ya plastiki akiwemo Asia Mgaya, Oneva Ilomo na Matrida Sanga wanasema mwamko umekuwa mdogo kwasababu vifungashio hivyo vimekuwa vikiuzwa kwa bei ya kuanzia elfu 2 hadi elfu tatu hatua ambayo inawafanya wateja kuacha kununua bidhaa kutokana na kukosa fedha ya kununua kifungashio.
Matumizi ya mifuko ya plastiki nchini yamekuwa yakifanyika vizazi na vizazi lakini katazo la serikali limepokelewa vipi na wanananchi na kudai kwamba wamekuwa wakipata wakati mgumu na kulazimika kubeba mkononi bidhaa wanazo nunua.
Nae Betrice Sanga ambaye ametumia katazo hilo kuwa fursa amebuni mradi wake vikapu mjini Njombe na kupata mwamko mkubwa wa wateja hapa anatoa mtazamo wake kuhusu ujasiriamali huo huku akiomba serikali kumuwezesha mtaji kwa kumpa mkopo wa riba nahafuu.