Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa, Mabalozi, Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali kabla ya kufungua Mkutano wa Haki, Amani na Maridhiano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma.
Viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa, baadhi ya Mabalozi wakiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma kuhudhuria Mkutano wa Haki, Amani na Maridhiano, ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Zitto Kabwe, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Bara) Abdulrahman Kinana katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama vya Siasa waliohudhuria Mkutano wa Amani, Haki na Maridhiano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Zitto Kabwe na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Bara) Abdulrahman Kinana wakitoka nje ya ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma baada ya kuzungumza na viongozi mbalimbali wa vyama vya Siasa waliohudhuria Mkutano wa Haki, Amani na Maridhiano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Zitto Kabwe, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM-Bara) Abdulrahman Kinana nje ya ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma baada ya kuzungumza na viongozi mbalimbali wa vyama vya Siasa waliohudhuria Mkutano wa Haki, Amani na Maridhiano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Jijini Dodoma
.…………………………………..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa vyama vya siasa na wadau wengine wa siasa kufanya majadiliano na kutoa mapendekezo ambayo yataleta maridhiano, haki na amani hapa nchini.
Rais Samia ametoa wito huo leo wakati akifungua Mkutano wa kitaifa wa haki, amani na maridhiano uliofanyika katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.
Aidha, Rais Samia amevitaka vyama bya siasa kufanya majadiliano kwa kuzingatia hali ya siasa, uchumi na mazingira halisi ya nchi kwa manufaa ya Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao.
Rais Samia pia amesema Tanzania ilichagua mfumo wa vyama vingi ili kuiwezesha kupata maendeleo kwa haraka hivyo, amewahakikishia kuwa Serikali itashirikiana na vyama vya siasa hususan katika masuala ya kisera na kisheria ili kuijenga nchi.
Vile vile, Rais Samia amekiagiza Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Kuangalia mfumo wa wajumbe wanaounda Taasisi hiyo ili kujumuisha wawakilishi kutoka ngazi zote za kisiasa na kuhakikisha wanafikia malengo yanayokusudiwa.
TCD ni Taasisi isiyo ya Kiserikali iliyoundwa na vyama vya siasa vyenye uwakilishi kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Mabaraza la Madiwani iliyosajiliwa mwaka 2005.