Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Ally Juma Makoa (Mb) akimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) (hayupo pichani) kwa ajili ya wasilisho kuhusu Programu ya Kuongeza Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu katika ukumbi wa Bunge wa Utawala Annex, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ambapo amewaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha miradi mbalimbali ya Wizara, katika ukumbi wa Bunge wa Utawala Annex, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akisisitiza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ambapo amewaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha miradi mbalimbali ya Wizara, katika ukumbi wa Bunge wa Utawala Annex, jijini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Programu ya Kuongeza Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu katika ukumbi wa Bunge wa Utawala Annex, jijini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Programu ya Kuongeza Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu katika ukumbi wa Bunge wa Utawala Annex, jijini Dodoma leo.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe.Hassan Mtenga (Mb) akiipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mafanikio yaliyopatikana kwenye Programu ya Kuongeza Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kilichofanyika ukumbi wa Bunge wa Utawala Annex, jijini Dodoma leo.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Asya Mohammed (Mb) akichangia mada wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kilichofanyika ukumbi wa Bunge wa Utawala Annex, jijini Dodoma leo.
………………………………………………..
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) ameahidi kutoa ushirikiano kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya Wizara.
Ameyasema hayo leo Aprili 3,2022 katika kikao cha Wizara cha kuwasilisha taarifa ya Programu ya Kuongeza Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Misitu kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika ukumbi wa Bunge wa Utawala Annex, jijini Dodoma.
“Mwenyekiti Mimi na Naibu Waziri tunaiahidi kamati hii ushirikiano wa hali ya juu, muda wowote tuko tayari, tutafika na kufafanua chochote mtakachohitaji, iwe ni habari ya kutoa elimu kuhusu jambo fulani ndio wajibu wetu” amesema Mhe. Chana.
Aidha, amefafanua kuwa ipo haja ya kamati hiyo kutembelea miradi yote ya Wizara ili kupata uelewa wa pamoja na kuweza kutoa mapendekezo ya kuiboresha.
Naye, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema kuwa Wizara imepokea maoni yote yaliyotolewa na kamati hiyo na itahakikisha inayafanyia kazi ili kukamilisha miradi ya Wizara.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa amesema kuwa lengo la Programu hiyo ni kuboresha mnyororo wa thamani na ushiriki wa sekta binafsi, kuimarisha uwezo wa wadau, kuendeleza elimu ya ugani, ufuatiliaji na tathmini na kuwezesha wizara katika uandaaji wa Sera, Sheria na Miongozo.
Amesema mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa programu hiyo inayogharimu shilingi bilioni 25, ni pamoja na kuandaa mipango ya usimamizi wa misitu, kuwezesha uvunaji wa mazao ya misitu, ununuzi wa mashine za kuchakata magogo na mitambo ya kukaushia mbao, ununuzi wa mizinga ya nyuki, pikipiki na mashine za kukaushia uyoga.
Programu hiyo inatekelezwa katika mikoa ya Tanga, Lindi na Ruvuma inatekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia kampuni ya Finland Consulting Group na imeanza mwezi Julai 2018 na inatarajiwa kukamilia mwezi Julai mwaka 2022.