Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali, Wanachama pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wakati akifunga Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika leo April 1,2022 Jijini Dodoma.
VIONGOZI mbalimbali wa Chama pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa ndani ya ukumbi wa Jakaya Kikwete kwa ajili ya kupitisha marekebisho ya Katiba ya Chama ya mwaka 1977 pamoja kumpigia kura kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana leo April 1,2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka kwa Wazee nchini kwa kutambua na kuthamini mchango wake mkubwa wa kuleta maendeleo nchini kabla ya kufunga Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika leo April 1,2022 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu Maalum uliofanyika leo April 1,2022 Jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo wakati akiondoka katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mara baada ya kufunga Mkutano Mkuu Maalum wa CCM leo April 1,2022 Jijini Dodoma.
………………………………………………………..
Na Alex Sonna, John Bukuku-DODOMA
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,amesema kuwa mabadiliko yaliofanyika katika Katiba ya Chama yanalenga kwenda sambamba na kufuata mifumo ya kisiasa katika dunia.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo April 1,2022 wakati akitoa hotobu yake kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika Jijini Dodoma.
Rais Samia amesema kuwa wamelazimika kubadili katiba hiyo ya mwaka 1977 kwa dhamira ya kukifanya Chama chenye nguvu nchini Tnazania na chenye kufuata siasa za kimataifa badala ya kubakia katika mfumo wa kisasa.
‘Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya CCM na hawawezi kubakia walipo sasa na ni vyema kamati za siasa zianze kujipanga kuona unakuwa wa uhuru na haki na sio kuwekeana visasi.’
”Mabadiliko hayo yanakusudia kuongeza ufanisi wa kazi za chama na sio kubakia walipo sasa, kwani wamerudisha mfuko wa kuwashirikisha Makatibu Wakuu kwenye Vikao vya Halmashauri kuu ili waweze kufuata maelekezo ya Chama yanapotolewa na sio wasubiri washushiwe.”amesema Rais Samia
Pia amesema kuwa malengo mengine ni kwa ajili ya kutafuta njia za kusimamia vyema mfumo wa serikali za mitaa kwani kumeonesha kuna kasoro katika kusimamia miradi ya chama katika ilani yake.