Ndoto ya Kufunga ndoa ya Kijana Yahya Said Khamis yapotea kwa muda ni baada ya nyumba yake kuungua Moto na vitu vyote vilivyokuwemo Ndani kuteketea ikiwemo vyombo vya mahari Pamoja na Shillingi Millioni Moja na nusu za Kitanzania.
Na, Hassan Msellem, Pemba +255672270730
Kijana Yahya Said Khamis mwenye umri wa miaka 23 Mkaazi wa Kijiji Cha Kichanjaani Shehia ya Dodo Pujini Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, amejikuta katika wakati mgumu baada ya nyumba yake kuungua na vitu vyote vilivyokuwemo Ndani kuteketea Kwa Moto vitu vyote vikikadiriwa kuwa na thamani ya Shillingi 2495000 za Kitanzania pamoja na kuathiri waya wa Umeme uliokuwa katika usawa wa paa la nyumba hiyo.
Tukio Hilo limetokea March 26 majira ya saa 2 na nusu za Usiku katika Kijiji Cha Kichanjaani Shehia ya Dodo Pujini.
Akizungumza na na Mwandishi wa Habari hizi Yahya amesema, wakati akiwa amekaa maskani na Vijana wenzake alisikia taarifa ya nyumba yake kuungua Moto ndipo alipokimbilia Kwa ajili ya kuuzima moto huo jambo ambalo lilishindikana kutokana na Moto huo kuwa kuwa mkubwa kiasi ya kutoweza kuzimika Kwa njia ya kawaida.
“Nilikuwa nimekaa maskani na Vijana wenzangu Mida kama ya saa 2 na nusu za Usiku ndipo akaja Kijana akaniambia kuwa nyumba Yako inaingua kabla sijainuka nikapigiwa simu nakuambiwa nyumba yangu inaungua nikakimbilia ili nikazime lakini nilipofika Moto ulikuwa umeshakuwa mkubwa Sana hata kufikika hapafikiki kwahivyo tukashindwa kuuzima na kuteketeza vitu vyote vilivyokuwemo Ndani ikiwemo kitanda, Godoro, Nguo zote, Viatu na pesa zilikuwa Shillingi Millioni Moja na nusu, kiukweli huu moto umeangamiza Kila kitu na Chanzo Chake Hadi sasa hatujakijua” alisema
Ramadhan Harhan Farjala ni Sheha wa Shehia ya Dodo Pujini amekiri kupokea taarifa za nyumba hiyo kuungua Moto pamoja na kutoa wito Kwa Jamii kuacha tabia ya kulipiziana visasi ambavyo vinagharimu Kwa kiasi kikubwa Maisha na upotevu wa Mali.
“Nakiri kupokea taarifa ya kuungua Moto nyumba ya Kijana Yahya Said Khamis juzi tarehe 26 Mwezi wa tatu Majira ya saa 3 usiku na kuteketeza Kila kitu kilichokuwemo ndani yani hizo nguo unazomuona nazo Said hapo mwilini mwake Hana nguo nyengine, wito wangu Kwa Jamii nawaomba tuache Tabia ya kulipiziana kisasi kwani sio tabia mzuri na inagharimu Sana Maisha na upotevu wa nguvu kazi Katika Jamii” alieleza
Tukio Hilo limesharipotiwa Katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake ili kifikishwa katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kitengo Cha maafa Kwa ajili ya msaada wa dharura Kwa Kijana huyo.
Hadi muda huu Chanzo Cha Moto huo hakijafahamika.