Rais Magufuli amemualika Rais Museveni wa Uganda katika ufunguzi wa mkutano mkubwa wa Wafanyabiashara kati ya Uganda na Tanzania ambao utawashirikisha wafanyabiashara zaidi ya 1000 ambao watapata nafasi ya kujadili namna ya kuongeza biashara mpya baina ya nchi hizi Mbili.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa wakati akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akihamasisha wafanyabiashara wa Tanzania kujitokeza Kwa wingi kushiriki katika kongamano hilo linalotaraji kufanyika Septemba 6,2019 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Bashungwa amesema kongamano hilo litafunguliwa na Rais Yoweri Museven wa Uganda litagudhuriwa pia na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli
Aidha Waziri Bashungwa Ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mikoa ya kanda ya ziwa ambao wengi wao ndio wamekuwa wakifanya biashara Moja kwa Moja na nchi za jirani hili waweze kupata mtandao mpya wa kibiashara.
Ametaja na kusema muungano wa kimtandao baina ya Tanzania na Uganda utafungua njia mpya ya Biashara hadi Sudan ya kusini ambao wamekuwa wakifanya biashara na Uganda kila uchwao.
Amesema muungano wa kibiashara baina ya nchi hizi Mbili utaongeza mabilioni kwa nchi yetu ya Tanzania kwani mpaka Sasa sisi ndio tumekuwa tukiuza zaidi kwao kuliko wao kuuza kwetu.
Amesema kuwa Uganda imekuwa ikitegemea mazao ya chakula kutoka hivyo wauzaji wa nafaka na Wasindikaji wa vyakula wanatakiwa kutumia fursa hii vizuri kwa kutanua masoko yao.