******************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua ACI. Hassan Ali Hassan, kuwa Kamishna wa Uhamiaji, Zanzibar. Kabla ya uteuzi huo ACI. Hassan alikuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba.
ACI. Hassan anachukua nafasi ya Kamishna Johari Masoud Sururu ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Uteuzi huu unaanza mara moja.