Mkuu Wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amewakikishia Wakazi Wa Tarafa ya Kiponzero kuwa kurejeshwa Kwa shughuli za kimahakama katika Kata ya Maboga hakutoathiri shughuli za kimahakama zinazoendelea kata ya Ifunda.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu Wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amewakikishia
Wakazi Wa Tarafa ya Kiponzero kuwa kurejeshwa Kwa shughuli za kimahakama katika
Kata ya Maboga hakutoathiri shughuli za kimahakama zinazoendelea kata ya
Ifunda.
Akizungumza na viongozi wa vijiji na kata za Tarafa ya Kiponzero
Mkuu wa Wilaya huyo alisema kuwa alipata malalamiko ya kuhamishwa kwa mahakama
kutoka Kiponzero kwenda Ifunda jambo ambalo limenipelekea kulifanyia kazi suala
hilo kushirikiana na mamlaka husika.
Alisema kuwa mahakama ya mwanzo Kiponzero itarudi na kufanya
kazi zake katika kijiji cha kiponzero kama ambapo ilikuwa awali na kuwahudumia
wananchi wote wa Tarafa ya Kiponzero
Moyo alisema kuwa kilichobakia ni makubaliano ya wananchi kuanza
kuchangia ujenzi wa choo na kukarabati jingo la mahakama ambapo kinatakiwa
kiasi cha shilingi milioni sita (6,000,000)
Alisema kuwa viongozi wa vijiji vyote kumi na tano wamekubali
kuchangia kiasi cha shilingi lakini nne (400,000) na mwisho wa michango ya
wananchi ni tarehe 30/4/2022 ili zoezi la ukarabati na ujenzi wa choo uanze
mara moja.
Moyo alisema kuwa Mahakama iliyopo Ifunda itaendelea na shughuli
zake Wakati huo huo Mahakama ya mwanzo ya Kiponzero pia itakuwa ikitoa huduma
kwa lengo la kusaidia wananchi kupata huduma za kimahakama kwa urahisi zaidi.
Alisema kuwa Tarafa ya Kiponzero inajiografia ngumu kidogo hivyo
serikali imeamua kuwa wananchi ambao wapo karibu na mahakama ya Ifunda
wataendelea kupata huduma za kimahakama Ifunda hivyo hivyo na wananchi waliopo
karibu na kijiji cha Kiponzero nao watapata huduma hiyo.
katika kikao hicho viongozi wa Tarafa hiyo wamekubaliana Kwa
pamoja Ili kufanikisha Ukarabati wa jengo la Mahakama ya Kiponzero Wananchi
watachangia kiasi cha shilingi milioni sita na kinachosalia kitatolewa
idara ya mahakama.
Aidha mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa
ametembelea ujenzi wa ofisi ya Afisa Tarafa ya Kiponzero na ujenzi unaendelea
vizuri na hivi karibuni ofisi hiyo itaanza kufanya kazi.
Moyo alisema kuwa baada ya wiki mbili wananchi wa Tarafa ya
Kiponzero wataanza kupata huduma kutoka kwa Afisa Tarafa katika makao makuu ya Tarafa
hiyo katika kijiji cha Kiponzero.
Aliwaomba wananchi kumuombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Samia Suhulu Hassan ili aweze kuwaletea maendeleo na huduma
zote muhimu karibu na wananchi.
Nao baadhi ya wenyeviti na watendaji wa vijiji,kata na Tarafa
hiyo wamesema kuwa wamefurahishwa na kitendo cha serikali ya awamu ya sita
chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suhulu Hassan
kuamua kuwasogezea huduma ya kimahakama karibu yao.
Walisema kuwa kulingana na ukubwa wa Tarafa hiyo kulikuwa
kunawatesa baadhi ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za
kimahakama ili kupata haki zao ambazo wanakuwa wanazidai kisheria.
Amina said ni m kazi wa kijiji cha Maboga alisema kuwa wamekuwa
wakinyimwa haki zao za msingi kwa kuwa mahakama ilikuwa mbali na maeneo yao
kiasi kwamba kesi nyingi walishindwa kuzifaatili kutokana na kutumia gharama
kubwa kufuata huduma hiyo.