Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoa kitambaa kuzindua mradi wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Majengo Tanzania TBA katika eneo la Magomeni Kota Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua mradi wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Majengo Tanzania TBA katika eneo la Magomeni Kota Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikabidhi mfano wa Ufunguo kwa Bibi Mwajuma Sama na Mzee Henry Ngwemba kwa ajili ya kuwakabidhi Nyumba mara baada ya kuzindua rasmi mradi wa Nyumba 644 Magomeni Kota Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua mradi wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Majengo Tanzania TBA katika eneo la Magomeni Kota Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Dar Es salaam baada ya kuzindua mradi wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Majengo Tanzania TBA katika eneo la Magomeni Kota Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Msanifu majengo Daud Kondoro wakati alipokuwa akitoa maelezo kuhusu hatua mbalimbali za Ujenzi wa Nyumba 644 katika eneo la Magomeni Kota Mkoani Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi wa Mkoa wa Dar Es salaam na Wakala wa Majengo Tanzania TBA baada ya kuzungumza na Wananchi na kuzindua mradi wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali kupitia TBA katika eneo la Magomeni Kota Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.
***************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuruhusu wananchi wa Magomeni Kota kuuziwa nyumba kwa utaratibu wa mpangaji ununuzi.
Rais Samia ametoa maelekezo hayo leo wakati akizindua nyumba 644 za makazi za Magomeni Kota Jijini Dar es Salaam ambazo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 52.
Wakazi hao ambao wameahidiwa kukaa bure kwa miaka mitano, wameruhusiwa kulipa gharama za ujenzi wa nyumba pekee bila ya gharama za ardhi na miundombinu ya jumuiya baada ya miaka hiyo.
Hata hivyo, wakazi wanaotaka kulipa gharama ya ununuzi kabla ya kufika miaka mitano wanaruhusiwa kulipa kidogo kidogo kwa kipindi cha miaka 10 bila ya riba yoyote.
Rais Samia amewasihi wakazi hao kutunza nyumba hizo na kuzingatia usafi wa ndani na nje na kuchangia huduma jumuishi kwa faida ya kila mmoja.
Aidha, Rais Samia amewataka TBA, NHC na Watumishi Housing kukaa na sekta binafsi ili kukubaliana katika ujenzi wa makazi bora kwenye maeneo yanayopaswa kuendelezwa.
Mahitaji ya nyumba bora yanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 3 nchi nzima, huku ongezeko la mahitaji ya nyumba bora ni takribani laki mbili kila mwaka.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Samia amefanya mazungumzo ya kushirikiana katika maendeleo mbalimbali hasa kwenye masuala ya miundombinu na nishati na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Africa50, Alain Ebobisse aliyeambatana na Ujumbe wake Ikulu, Jijini Dar es Salaam.