*****************
Na Mahanga the Great-Katavi.
Wakazi wa Kata ya Mishamo Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi sasa wameondokana na Vifo vya Mama wajawazito visivyotarajiwa baada ya kukamilika kwa Ujenzi wa Majengo 6 ikiwemo chumba Upasuaji katika Kituo cha Afya cha Mishamo iliyogharimu shilingi milioni 400 zilizotolewa na Serikali huku Wananchi wakitolea nguvu kazi kwa kufyatua Tofali.
Wakiongea kituoni hapo baadhi ya Wananchi wameeleza furaha yao kufuatia kukamilika kwa kituo hicho ambapo awali walilazimika kusafiri zaidi ya km 140 kufuata huduma Hospitali ya Rufaa teule ya Mkoa wa Katavi pindi mgonjwa napokuwa na hali mbaya kutokana na kukosekana kwa Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mbwana Mhando amebaibainisha kuwepo kwa Changamoto ya Maji Safi na Salama Pamoja na Nishati ya Umeme katika Kituo hicho hali inayopelekea Kukwama kwa Huduma kama ilivyokusudiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera ameahidi kutafuta wadau watakaowezesha kusaidia kutatua changamoto hizo ambazo wanakabiliwa nazo katika Kituo cha Afya cha Mishamo.