Mkuu Wa Mkoa wa Simiyu Wapili kushoto akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya Ulinzi ya Mkoa pamoja na mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Lupakisyo Kapange wakati wa ziara ya ujenzi barabara ya Byuna/Nkindwabiye na Halawa, bariadi yenye urefu wa Km 139.993 mln
**************************
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila ametoa siku saba kwa Kampuni ya Daska Company Ltd, kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa Barabara ya Byuna/Nkindwabiye/ Halawa barabara yenye urefu wa 14.9km. Thamani ya mradi/mkataba huo ni Tsh.139.993 mln.
“Tofauti na hapo mkataba uvunjwe na taratibu zifuatwe kupata kampuni nyingine.Sina na sijawahi kuwa na subira kwa wakandarasi wababaishaji. Nitoe wito Wakandarasi wote mkae mguu sawa. Nitafuta kazi zote zinazosuasua ili kubaki na wakandarasi wenye uwezo wa kutekeleza kazi kwa mujibu wa mikataba wanayosaini”.Amesema Kafulila.
Kafulila ametoa maelekezo hayo kwa Meneja wa Mkoa wa Mamlaka ya Barabara vijijini( TARURA) wakati wa ziara yake leo Machi14, 2022 wilaya ya Bariadi.