Wakazi wa Boko jijini Dar es Salaam wakisoma vipeperushi vya Mahakama Inayotembea wakati gari maalum la Mahakama hiyo lilipokuwa likitoa elimu kwa umma kuhusu Mahakama hiyo.
Karani wa Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Nise Mwasalemba(mwenye shati la njano ndani ya gari hilo maalum ) akitoa elimu kwa umma kuhusu Mahakama Inayotembea na shughuli zitakazofanywa na Mahakama hiyo, kwa wakazi wa Boko Magengeni, jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji wa elimu kwa Umma.
Wananchi wakipatiwa elimu kuhusu Mahakama Inayotembea na Karani Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Nise Mwasalemba ndani ya gari hilo maalum lililokuwa limepaki eneo la Ofisi ya Mtendaji Kata ya Bunju