Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania Dkt. Daniel Mushi akizungumza na waandishi wa habari akieleza ni namna gani wanaweza wakashiriki katika Tamasha la Ulaji wa Nyama la ‘Kuku Choma Carnival’ linalotarajiwa kufanyika April 17 na 18 Jijini Dar es salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Gulu Planet Limited Bw.Nikson Magezi akizungumza na waandishi wa habari akieleza ni namna gani wanaweza wakashiriki katika Tamasha la Ulaji wa Nyama la ‘Kuku Choma Carnival’ linalotarajiwa kufanyika April 17 na 18 Jijini Dar es salaam. Baadhi ya wadau wa nyama wakiwa kwenye mkutano huo
**********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Ulaji wa Nyama la ‘Kuku Choma Carnival’ linalotarajiwa kufanyika April 17 na 18 Jijini Dar es salaam mwaka huu lenye lengo la kuhamasisha ulaji wa nyama na uzalishaji.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania Dkt. Daniel Mushi amesema katika tamasha hilo wamepanga kuwaleta pamoja wadau wanaozalisha mifugo na nyama na wachakataji.
“Tunaendelea kutoa fursa kwa makampuni kuungana nasi katika Tamasha hili, tayari kuna baadhi ya makampuni yameshaungana nasi na vilevile kwenye hili tamasha wananchi tunawakaribishwa kwani ni bure kabisa”. Amesema Dkt.Mushi
Dkt.Mushi amesema Bodi ya Nyama itaendelea kutafuta Masoko mapya lakini pia kuendeleza tasnia ya nyama kwa kuwapa elimu wadau mbalimbali ili kuwahamasisha ufugaji bora wa kisasa huku akieleza kuwa watanzania kwa wasatani wanakula nyama kilo 15 kwa mwaka.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Gulu Planet Limited Bw.Nikson Magezi amesema wanajaribu kukutanisha wadau wakuu ambao ni wazalishaji wa vifaranga, Wazalishaji wa vyakula na wadau wengiine mbalimbali wakutane na mfugaji moja kwa moja na kuweza kuhakikisha mfugaji anapata fursa na kuzitumia akiwa amelenga soko na kuweza kuzalisha ajira.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa TABROFA ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji wa Kuku Kinondoni (WAKUKI) Aloyce Makoye wamekuwa wakiwaelimisha wateja wao kuwa kuku wanyama hawana madhara lakini pia wanafanya uboreshaji wa uzalishaji.