Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makiragi akitoa vyeti kwa wahitimu walioshiriki mafunzo ya siku tano ya UVIKO !( kwa wadau wa Sekta ya Utalii yaliyotolewa na Chuo cha Taifa cha Utalii Machi 11-2022, Jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makiragi akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya kufunga rasmi Mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kuuudhuriwa na wadau zaidi ya 170 kutoka katika Wilaya zote za Mkoa huo.
kurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chuo cha Taifa Cha Utalii, CPA. Munguabela Kakulima akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya utangulizi akimuwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka wakati wa hafla ya kuyafunga rasmi Mafunzo hayo Jijini Mwanza.
Mratibu wa Mafunzo katika Jiji la Mwanza Dkt. Cuthbert Mero akitoa salamu zake kwa mgeni rasmi na kufanya utambulisho kwa wageni mbalimbali waliofika ku |
Mhadhli Mwandamizi wa Chuo cha Taifa cha Utalii Elina Makanja akizumza alipokuwa akiongoza ratiba katika hafla hiyo.
Mratibu wa mafunzo, na msimamizi mkuu wa Mradi wa mafunzo hayo Dkt. Naiman Mbise akieleza namna ambayo Chuo cha Taifa cha Utalii kilivyotekeleza kikamilifu shughuli nzima ya utoaji wa mafunzo hayo katika mikoa nane ya Tanzania Bara. (PICHA NA HUGHES DUGILO)
Na: Hughes Dugilo, MWANZA.
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imekamilisha mafunzo ya UVIKO 19 kwa wadau wa Sekta ya Utalii yaliyokuwa yakitolewa katika mikoa nane ya Tanzania Bara kupitia MPANGO WA MAENDELEO KWA USTAWI WA TAIFA NA MAPAMBANO DHIDI YA UVIKO 19.
Mafunzo hayo yaliyokuwa yakitolewa na Chuo Cha Taifa cha Utalii yalilenga kuwajengea uwezo wadau waliopo katika mnyororo wa Sekta hiyo kwa
kuwa wengi wao hawana weledi wa utoaji huduma hasa wakati huu wa janga
la UVIKO-19, hivyo mafunzo hayo yatawawezesha kujikinga wao wenyewe pamoja na wageni wanaopata huduma
zao sambamba na kuboresha huduma zao ili thamani ya pesa inayotolewa na mgeni
au mtalii iweze kuonekana.
kuwa wengi wao hawana weledi wa utoaji huduma hasa wakati huu wa janga
la UVIKO-19, hivyo mafunzo hayo yatawawezesha kujikinga wao wenyewe pamoja na wageni wanaopata huduma
zao sambamba na kuboresha huduma zao ili thamani ya pesa inayotolewa na mgeni
au mtalii iweze kuonekana.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo katika Mkoa wa Mwanza ambapo pia hafla hiyo ilikwenda sambamba na kuhitimisha rasmi awamu ya kwanza ya mafunzo hayo katika mikoa yote nane, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii na Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Chuo hicho CPA Munguabela Kakulima amesema kuwa kumekupo na mafanikio makubwa Katika Mafunzo hayo na kwamba zaidi ya wadau 1700 wamefikiwa.
“Mafunzo haya yamefanyika kwa mafanikio makubwa sana ambapo wadau zaidi ya 1700 wamenufaika nayo, ni Imani yangu kuwa wadau wote waliopata mafunzo haya watakwenda kufanyakazi zao vizuri kwa kufuata yale waliyoyapata kwenye mafunzo haya” Aliongea Kakulima.
Aidha ameeleza namna ambavyo mafunzo hayo yalivyoamsha hamasa kwa wadau wote walioshiriki mafunzo hayo na kwamba wapo miongoni mwao walioonesha nia ya kutaka kujiunga na Chuo cha Taifa cha Utalii ili kujiendeleza zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makiragi akizungumza wakati wa kufunga rasmi mafunzo hayo amewataka wadau wote waliopata mafunzo hayo kutumia vema ujuzi huo katika kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini hususani katika Jiji la Mwanza ambapo kuna vivutio vingi vinavyohitajika kutangazwa hivyo kuwataka wadau hao kujikita katika kuvitangaza Vivutio hivyo.
Amewaeleza wadau hao kuwa elimu waliyoipata katika siku tano walizokaa Jijini Mwanza ikawe chachu ya kuendelea kutafuta fursa mbalimbali katika sekta ya Utalii ili kuongeza wigo wa shughuli zao katika kujiongezea kipato.
Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo hayo Dkt. Naiman Mbise kutoka Chuo Cha Taifa cha Utalii amempongeza Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha
hizo ambazo zimewezesha kuendesha mafunzo hayo katika kukabiliana na janga la VIKO 19 na kwamba Chuo hicho kimefanikiwa kufikia malengo yake katika kusimamia na kutoa mafunzo hayo kwa mikoa yote nane ambapo mafunzo hayo yamehitimishwa rasmi Machi 11,2022 katika mikoa ya Mwanza na Mara.
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha
hizo ambazo zimewezesha kuendesha mafunzo hayo katika kukabiliana na janga la VIKO 19 na kwamba Chuo hicho kimefanikiwa kufikia malengo yake katika kusimamia na kutoa mafunzo hayo kwa mikoa yote nane ambapo mafunzo hayo yamehitimishwa rasmi Machi 11,2022 katika mikoa ya Mwanza na Mara.
“Kwakweli Chuo limefikia malengo yake katika kutoa mafunzo haya, nipende kuwashukuru watumishi wote wa Chuo kwa kufanyakazi hii kwa weledi mkubwa mpaka kufikia tamati, pia wadau wote wa Sekta ya Utalii waliojitokeza kupata mafunzo haya, naamini yatakwenda kuleta mabadiliko makubwa ya utoaji wa huduma katika shughuli zao. Alisema Dkt. Mbise.
Mafunzo hayo ya UVIKO 19 kwa wadau wa Sekta ya Utalii yamefikia tamati ikiwa ni awamu ya kwanza katika Mikoa nane ya Tanzania Bara ikiwemo, LINDI, MTWARA, RUVUMA, NJOMBE, IRINGA, MBEYA, MWANZA NA MARA.
TAZAMA VIDEO
PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO KATIKA MAFUNZO HAYO.