*********************
Baadhi ya viongozi wa Serikali na Taasisi mbalimbali nchini katika picha akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania ( TET) Dkt. Aneth Komba wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati alipokuwa akiwahutubia leo tarehe 07 Machi, 2022 katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Benjamini William Mkapa.
Katika hotuba hiyo Mhe. Rais ameahidi kuhakikisha kuwa serikali inaweka mazingira bora ya kuwafanya watoto wote nchini kupata elimu na kwamba hakuna mtoto yeyote atakayeachwa nyuma.
Aidha Mhe. Rais ametaja mambo mbalimbali yaliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita yenye lengo la kutoa elimu bora kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu. baadhi ya mambo hayo ni pamoja na kusambaza vitabu vya maandishi ya Breli na maandishi yaliyokuzwa kwa wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu wa darasa la kwanza hadi la saba.
Vilevile, amesema kuwa serikali imetoa shilingi 706,998,580.50 kwa ajili ya vitabu vya Breli na maandishi yaliyokuzwa kwa masomo mbalimbali kwa Kidato cha Kwanza hadi cha Nne.