Naibu waziri wa Nishati Bi Subira Mgalu akiwa tayari kwa ajiri ya kukata utepe kwenye nyumba ya Bi Asha Rashidi Iliounganishwa umeme wa Rea awamu ya tatu, wakwanza kutoka kulia ni Mbunge wa kilosa Mhe Ahmed Bawazi.
Naibu waziri wa Nishati Bi Subira Mgalu akiongea na wananchi wa vijiji vya Kitati na Kidete wilayani Kilosa Mkoani Morogoro baada ya kusimamishwa kwa msafara wake.
Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mhe Ahmed Bawazir akijibu kelo za wananchi wa Ludewa waliojitokeza kwenye mkutano kufuataia ziara ya Naibu Waziri wa Nishati Bi Subira Mgalu..
………………………………..
NA FARIDA SAIDY,MOROGORO
Wananchi wa vijiji vya Kitati na Kidete Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro wamezuia kwa muda msafara wa Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu wakishinikiza kupelekewa umeme kwenye vijiji vyao licha ya vijiji jirani vya Wilaya ya Mpwapwa kuwa na umeme kwa kila nyumba huku wao wakiendelea kuteseka na giza hali inayopelekea wananchi wa vijiji hivyo kuendelea kuwa masikini
Wakizungumza kwa masikitiko baada ya kuzuia msafara huo wananchi hao wameeleza kusikitishwa na hatua ya vijiji jirani vya Wilaya ya Mpwapwa kuwa na umeme kila nyumba licha ya kuwa na Zahanati pamoja na shule ambazo zinahitaji umeme jambo ambalo linafanya Baadhi ya huduma za kiafaya kuwa za kusuasua kwa kuwa zinategemea umeme.
Katika hatua nyingien akiwa katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Dundumwa wananchi hao waliazisha vurugu wakilalamikia maafisa wa REA kubagua baadhi ya nyumba za kuziweekea umeme,ambapo swala hilo lilimlizimu Mbunge wa jimbo la kilosa Ahmed Bawazir kutuliza vurugu hizo kwa kuwalipia fedha baadhi yao ili wawekewe umeme kwenye vijiji vyao
Katika ziara yake wilayani kilosa Naibu Waziri Mgalu amefanya mikutano na wananchi katika kijiji cha Kidete, Lumuma na baadae kuwasha umeme katika kijiji cha Dundumwa kata ya Ludewa na kuongea na wananchi.