Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), kilichofanyika leo Februari 26,2022 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis akieleza jambo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), kilichofanyika leo Februari 26,2022 jijini Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akieleza lengo la kikao kazi cha Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili kwa Wanawake na Watoto kilichofanyika jijini Dodoma
Kaimu Mkurugenzi Mkaazi wa Plan International Peter Mwakabwale, akielezea jinsi wanavyotekeleza kwa kushirikiana na Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili kwa Wanawake na Watoto kilichofanyika jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Vickness Mayao akieleza jinsi Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anavyoshirkiana katika afua za kutokomeza ukatili wakati wa kikao kazi cha Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili kwa Wanawake na Watoto kilichofanyika jijini Dodoma.
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania (NGOs) Neema Lugangira,akizungumza katika kikao kazi cha Wadau wanaotekeleza afua za kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto,kilichofanyika leo Februari 26,2022 jijini Dodoma
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Wadau wanaotekeleza afua za mpango kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakifuatilia matukio mbalimbali katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akiitunza Kwaya ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakati ikitumbuiza kwenye ufunguzi wa kikao kazi cha Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), kilichofanyika jijini Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), kilichofanyika jijini Dodoma
………………………………………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima,amewataka wadau kushirikiana na Serikali kufanya oparesheni maalum ya kuwaondoa watoto wa mtaani na kuzuia ukatili majumbani.
Dk.Gwajima ameyasema hayo leo Februari 26,2022 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi na Wadau waotekeleza afua za kupambana na vitendo vya ukatili nchini.
Amesema kuwa kikao hicho cha kazi kitajielekeza kwenye kujadili na kupata majibu ya kutumia mbinu gani kuzuia ukatili wa majumbani kwa watoto na wanawake na pia ni mbinu gani za kunusuru watoto walio wahanga wa ukatili kukimbilia kuishi na kufanya kazi mitaani na wanawaondoaje waliopo mtaani sasa.
“Tujadili na kukubaliana juu ya hatua zipi zinahitajika kuchukuliwa kwenye operesheni ya kudhibiti ukatili majumbani na operesheni ya kuzuia watoto wasikimbilie mitaani na pia operesheni ya kuwaondoa watoto walio mtaani sasa,”amesisitiza
Awali Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk.Zainab Chaula,amesema lengo la kikao hicho ni kutaka kujua mikakati gani waliojiwekewa wadau katika kukabiliana na vitendo vya ukatili.