Meneja wa shirika la umeme Tanesco mkoani Arusha,Mhandisi Herini Mhina akizungumza katika mkutano huo katika kata za Muriet na Terrat mkoani Arusha.
Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini,Mrisho Gambo akizungumza na Wananchi kwenye mkutano huo wa kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili .
***********************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Zaidi ya wananchi 128 kutoka kata za Terrat na Muriet mkoani Arusha wanatarajiwa kuondokana na adha ya ukosefu wa umeme baada ya shirika la umeme Tanesco kuanza rasmi mchakato wa kuwafungia umeme wateja wote waliolipia ndani ya siku saba.
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha Justin na Meneja wa TANESCO mkoa wa Arusha ,Mhandisi Herini Mhina wakati akizungumza na wananchi alipotembelea katika kata za Terrat na Muriet na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi hao.
Mhandisi Mhina amesema kuwa, wamezindua rasmi kampeni ya kumaliza wateja waliolipia ambao walikuwa wanasubiria kuunganishwa kwa gharama ya 27,000 katika kata hizo ,ambapo kampeni hiyo itafanyika katika kata zingine ambazo tayari wananchi wake walishalipia na wanasubiri kuunganishwa.
“Katika kata hizo mbili hadi kufikia desemba mwaka Jana wananchi hao 128 walishalipia umeme,ambapo Muriet tayari wananchi 75 walishalipia huku kwa kata ya Terrat wakiwa wananchi 53 ambao tayari wamelipia na ndani ya siku Saba wananchi wote watakuwa wameshapatiwa umeme na kuondokana na adha waliyokuwa nayo kwa muda mrefu”amesema .
Mhina amewataka wananchi hao waliokwisha kulipia na wanasubiri kufungiwa umeme kujiandaa kuwapa ushirikiano wataalamu wa TANESCO ambao wataweka nguvu wiki nzima kuhakikisha wananchi hao wamepata umeme na lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha wananchi wanapata umeme na kuondokana na changamoto mbalimbali .
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Mrisho Gambo amesema kuwa ,akizungumza na wananchi hao amewataka kufanya matayarisho mahususi ikiwa ni pamoja na kufanya wearing katika nyumba zao na ambao hawajalipia walipie ili waweze kupata huduma na kazi kuwa rahisi zaidi.
“Kwa kweli nampongeza Sana Rais Samia kwa namna ambavyo anafanya maendeleo katika maeneo mbalimbali kwani hizi zote ni juhudi zake kwani wananchi hawa wa Mkonoo wamekuwa wakilia umeme kila siku na tangu wapate Uhuru hawajawahi kupata umeme mdogo ,hivyo serikali ya Mama Samia kupitia TANESCO wameweza kupata umeme ni jambo kubwa Sana na la kumpongeza Rais wetu.”amesema.
Kwa upande wao wananchi wakizungumza katika mkutano huo,walipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na TANESCO la kuwaletea umeme kwani tangu wapate Uhuru hawajawahi kupata umeme ,hivyo uwepo wa umeme huo utarahisisha Sana Kasi ya maendeleo katika kata hiyo.
Elias Saigilu na Rose Mollel wananchi wa Kata ya Terrat Mkonoo wamesema kuwa, wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na ukosefu wa huduma ya umeme ambapo uwepo wa umeme huo utawezesha kujengwa kwa kituo cha afya na kuondoa adha ya kutembelea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.