Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Sama Lukonde ofisini kwa Waziri Mkuu huyo, Jijini Kinshasa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpatia zawadi ya picha ya clima Kilimanjaro, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Sama Lukonde baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu huyo, Jijini Kinshasa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya kinyago kutoka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu huyo, Jijini Kinshasa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Sama Lukonde baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu huyo , Jijini Kinshasa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sama Lukonde kuhusu picha mbalimbali za viongozi waliowahi kuiongoza nchi hiyo, baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu huyo, Jijini Kinshasa
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Tanzania na Kongo zimepanga kuandaa mkutano mkubwa wa pamoja kati ya wafanyabiashara wa nchi hizo ili kuzungumzia mwelekeo wa kibiashara.
Amesema kuwa mkutano huo ambao utajadili changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo wafanyabiashara wa nchi mbili hizo na namna ya kuzitatua utasaidi kuchochea uchumi wa kitaifa na wa mtu mmoja mmoja.
Amesema hayo jana (Februari 25, 2022) baada ya mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sama Lukonde yaliyofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu huyo jijini Kinshasa.
“Tuna fursa katika ziwa Tanganyika ambapo Tanzania tumejenga bandari tano muhimu zinaoweza kutumiwa na DRC, pia tuna barabara tunayoitumia kutoka Tunduma kwenda Kaprimposhi-Kasumbalesa, tunataka kubadilisha “route” ipite kwenye daraja la Kasenga barabara ambayo ni fupi sana inapunguza zaidi ya kilomita 2000 kwenda na kurudi.
Mheshimiwa Majaliwa amesema wamekubaliana kutembeleana ili kuimarisha utendaji na ufutiliaji pamoja na kuimarisha uhusiano.
Awali, Waziri Mkuu alikutana na watumishi katika ubalozi wa Tanzania nchini DRC na aliwataka kuongeza ubunifu ili kukuza diplomasia ya uchumi kati ya nchi hiyo na Tanzania.
“Tunapozungumzia ubalozi maana yake tunawataka muimarishe diplomasia yetu , ongezeni ubunifu ili tuweze kunufaika na mahusiano haya”
Mheshimiwa Majaliwa amerejea nchini baada ya kumalizika kwa mkutano wa kumi wa wakuu wa nchi na serikali kuhusu Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano na DRC pamoja na Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu uliofanyika jijini Kinshasa, ambapo alimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.