Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Julishaeli Mfinanga akizungumza na Watumishi wa Jengo la Kambarage tower baada ya kuhitimisha zoezi la Utayari kwa watumishi wa Jengo la Kambarage tower Jijini Dodoma leo tarehe 25 Februari, 2022, lengo la zoezi hilo ni kutathimini uelewa na utayari wa kukabiliana na majanga ya moto, maokozi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu)
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma wakiwa wamembeba majeruhi wa kuigiza wakati wa zoezi la Utayari kwa watumishi wa Jengo la Kambarage tower Jijini Dodoma leo tarehe 25 Februari, 2022, lengo la zoezi hilo ni kutathimini uelewa na utayari wa kukabiliana na majanga ya moto, maokozi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu)
Baadhi ya watumiaji wa Jengo la Kambarage tower, wakiwa eneo salama baada yakutoka ndani ya Jengo hilo wakati wa zoezi la Utayari kwa watumishi wa Jengo hilo Jijini Dodoma leo tarehe 25 Februari, 2022, lengo la zoezi hilo ni kutathimini uelewa na utayari wa kukabiliana na majanga ya moto, maokozi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu)
**********************
DODOMA FEBRUARI 25, 2022
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefanya zoezi la Utayari kwa watumishi wa Jengo la Kambarage tower Jijini Dodoma, lengo la zoezi hilo ni kutathimini uelewa na utayari wa kukabiliana na majanga ya moto, maokozi.
Mazoezi kama haya hufanyika mara kwa mara lengo likiwa kuwakumbusha na kuwapima watumiaji wa jengo jinsi gani wanavyoweza kupokea taarifa ya tukio la moto, wanawezaje kutoa taarifa sahihi na za uhakika kwa watoa huduma
Kwa upande wake Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Julishaeli Mfinanga aliwatoa hofu Wananchi kuwa zoezi hilo lilikuwa lakawaida na kuwakumbusha matumizi sahihi ya namba ya dharura ya Jeshi hilo 114 pindi wanapopatwa na majanga kwani wanapotoa taarifa mapema na kwa wakati ndipo watakapofikiwa haraka na Maisha na Mali vitaokolewa.
Aidha Meneja wa Tawi la Benki ya NMB Kambarage tower Bi. Emiliana Willison alilishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kufika mapema mara baada ya kupata taarifa na kuwahakikishia wateja na Wananchi kwa ujumla kuwa Benki hiyo iko salama na huduma zimerejea kama kawaida.