Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akitazama baadhi ya vinywaji vilivyotengenezwa na Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd mara baada ya kutembelea kiwando hicho kilichopo kiwalani Jijini Dar es Salaam. Waziri Jafo amefanya ziara ya kikazi leo 24/02/2022 ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira kufuatia marufuku iliyotolewa na Serikali Oktoba mwaka jana ya matumizi ya plastiki laini kwenye vifuniko vya chupa za maji (plastic seal). Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd Bw. Chengal Reddy mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho leo.Waziri Jafo amefanya ziara ya kikazi leo 24/02/2022 ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira kufuatia marufuku iliyotolewa na Serikali Oktoba mwaka jana ya matumizi ya plastiki laini kwenye vifuniko vya chupa za maji (plastic seal). Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akieleza jambo mbele ya watumishi wa Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd. Waziri Jafo amefanya ziara ya kikazi leo 24/02/2022 ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira kufuatia marufuku iliyotolewa na Serikali Oktoba mwaka jana ya matumizi ya plastiki laini kwenye vifuniko vya chupa za maji (plastic seal). Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza katika kikao na baadhi ya viongozi wa Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd mara baada ya kufanya ziara kwenye kiwanda hicho leo 24/02/2022 ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira kufuatia marufuku iliyotolewa na Serikali Oktoba mwaka jana ya matumizi ya plastiki laini kwenye vifuniko vya chupa za maji (plastic seal). Meneja wa Rasilimali Watu katika Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd akizungumza mbele Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo baada ya waziri huyo kufanya ziara kwwenye kiwanda hicho.Waziri Jafo amefanya ziara ya kikazi leo 24/02/2022 ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira kufuatia marufuku iliyotolewa na Serikali Oktoba mwaka jana ya matumizi ya plastiki laini kwenye vifuniko vya chupa za maji (plastic seal). Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd Bw. Chengal Reddy mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho leo.Waziri Jafo amefanya ziara ya kikazi leo 24/02/2022 ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira kufuatia marufuku iliyotolewa na Serikali Oktoba mwaka jana ya matumizi ya plastiki laini kwenye vifuniko vya chupa za maji (plastic seal). Moja ya mashine ya kuyatibu maji ambayo yatatumika kutengenezea vinywaji kwenye Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipokelewa na baadhi ya viongozi wa Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd mara baada ya kuwasili kwenye kiwanda hicho kwaajili ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira kufuatia marufuku iliyotolewa na Serikali Oktoba mwaka jana ya matumizi ya plastiki laini kwenye vifuniko vya chupa za maji (plastic seal).Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd Bw. Chengal Reddy wakati akimuelezea kuhusu mashine ya kuchakata chupa za vinywaji. Dkt Jafo amefanya ziara ya kikazi leo 24/02/2022 ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira kufuatia marufuku iliyotolewa na Serikali Oktoba mwaka jana ya matumizi ya plastiki laini kwenye vifuniko vya chupa za maji (plastic seal).
************************
Serikali imesema kamwe haitakuwa kikwazo kwa wawekezaji wanaolenga kuwekeza katika sekta ya viwanda bali maendeleo ya viwanda ni lazima yaende sambamba na hifadhi ya Mazingira.
Rai hii imetolewa leo Februari 24, 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo katika ziara ya kikazi ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira katika Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Dkt. Jafo amesema Serikali inahimiza wawekezaji nchini lakini ni vema wawekezaji hao wazingatie Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kwa ukamilifu wake. Katika ziara ya kukagua kiwanda hicho kinachozalisha vinywaji baridi (soda, maji na juisi).
Waziri Jafo amepongeza utii wa Kiwanda hicho kwa kutekeleza kwa wakati maagizo ya Serikali ya kutotumia karatasi za plastiki kwenye vifuniko vya chupa za maji.
“Kiwanda hiki kimenifurahisha sana, wametii kwa vitendo maagizo ya Serikali ya kutotumia karatasi za plastiki kwenye vifuniko vya chupa za maji yanavyozalishwa na Kiwanda hiki. Kiwanda hiki pia kimeanzisha kiwanda cha kurejeleza chupa za plastiki, hata zile za rangi ambazo ukusanyaji wake umekuwa na changamoto, natoa rai kwao kuhakikisha chupa zao hazisambai katika mazingira bali wanazirejesha kiwandani na kutengeneza bidhaa nyingine” Dkt. Jafo alisisitiza
Amesema, viwanda vina mchango mkubwa sana katika kukuza uchumi wa nchi sambamba na kuchangia ajira za moja kwa moja hivyo Serikali itahakikisha matakwa ya Sheria yanazingatiwa.
Naye Meneja wa Kanda ya Kusini Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Hamadi Taimur amesema kuwa watahakikisha wanasimamia maelekezo yote yaliyotolewa.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha A One product and Bottles Ltd Bw. Chengal Reddy amesema wamefanya jiitihada za dhati katika kuhakikisha chupa za rangi zinazozalishwa kiwandani hapo zinarudi katika mzunguko kwa kutengeneza bidhaa nyingine.
“Tuna kiwanda kingine Mbagala ambapo chupa hizi za rangi zinachakatwa na kutengeneza bidhaa nyingine za plastiki kama vile Busati na shedi za Magari” Alisisitiza Bw. Reddy.
Mapema mwezi Oktoba 2021 Serikali ilipiga marufuku matumizi ya plastiki laini kwenye vifuniko vya chupa za maji (plastic seal) na vinywaji baridi kwani ni hatari kwa mazingira na viumbe hai kwa kuwa hazirejelezeki na kuathiri ikolojia ya raslimali maji na ardhi.