Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na timu ya wataalam wanaoandaa mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Iringa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo huo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini, Bw. Hassan Kitenge na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango.
Mkurugenzi wa Idara ya Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini, Bw. Hassan Kitenge akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na timu ya wataalam wanaoandaa mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Iringa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa na timu ya wataalam wanaoandaa mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Iringa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza maelezo mafupi ya namna ya kujaza fomu iliyokuwa ikitumika awali ya Utendaji Kazi na Tathmini katika Ngazi ya Mtumishi (OPRAS) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Iringa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango (katikati) akimuelezea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama namna mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma utakavyokuwa ukifanya kazi wakati Waziri huyo alipowatembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa mfumo huo Mkoani Iringa.
Mmoja wa timu ya wataalam wanaoandaa Mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma, Bw. Michael Moshiro (wakwanza kulia) kutoka Chuo cha Mipango Dodoma akitoa maoni yake kuhusu ujenzi wa mfumo huo mpya kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo Mkoani Iringa iliyolenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na timu ya wataalam wanaoandaa mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Iringa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo huo.
…………………………………………………………
Na. Veronica Mwafisi-Iringa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama, amewataka Wataalam wanaotengeneza Mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kujenga mfumo rafiki na wenye uhalisia kati ya mtumishi anayefanyiwa na anayefanya tathmini ili kuleta tija kwa taifa.
Waziri Jenista ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Iringa ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma ambao umeanza kutekelezwa hivi karibuni na wataalam wa ndani kufuatia maelekezo ya Mhe. Rais ya kuubadilisha Mfumo wa awali wa Utendaji Kazi na Tathmini katika Ngazi ya Mtumishi (OPRAS) ambao alikuwa haridhishwi nao kiutendaji.
Pamoja na maelekezo ya Mhe. Rais, Mhe. Jenista amewataka wataalam hao kujenga mfumo utakaochochea uwajibikaji wa hiari kwa kila mtumishi badala ya kufanya kazi kwa mazoea na kwa kulazimishwa.
“Tujenge mfumo ambao kila mtumishi wa umma ataona fahari ya kufanyiwa tathmini kwa kuwajibika kwake kikamilifu na ajione yeye mwenyewe kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya taifa.” Mhe. Jenista amesisitiza.
Mhe. Jenista ameongeza kuwa, mfumo mpya wa Usimamizi wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma unaojengwa hivi sasa unatakiwa kuwa chachu kwa watumishi wa umma kupenda kufanyiwa tathmini kwa utendaji kazi wao mzuri ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada kubwa anazozifanya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan za kutafuta rasilimali fedha kwa lengo la kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi.
“Mhe. Rais amekuwa na jitihada kubwa katika kutafuta rasilimali fedha, hivyo tujenge mfumo ambao watumishi wenyewe watajikuta wanapenda kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili kuitendea haki rasilimali fedha anayoitafuta Mhe. Rais kwa lengo la kuleta matokeo chanya katika nchi yetu” Mhe. Jenista amesisitiza.
Mhe. Jenista ameipongeza Menejimenti ya Ofisi yake kwa kuzingatia maelekezo yake ya kuunda timu ya wataalam ya kujenga mfumo huo na kuielekeza timu hiyo kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuboresha zaidi mfumo huo.