Mkuu wa shule ya St. Mary’s tawi la Mbezi Beach Ntipoo Recka akizungumza wakati wa kikao hicho na kueleza kuwa kujituma kwa walimu, nidhamu ya wanafunzi na ushirikiano bora kutoka kwa wazazi kunaendelea kuiweka shule hiyo katika nafasi nzuri katika elimu, leo jijini Dar es Salaam.Makamu Mkuu wa shule ya St. Mary’s tawi la Mbezi Beach Rajabu Balele akizungumza wakati wa kikao cha wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo na kueleza kuwa wapo imara katika kuhakikisha ufaulu wa wanafunzi wa shule hiyo unakuwa zaidi, leo jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa bodi wa shule za St. Mary’s Dallas Mhoja akizungumza wakati wa kikao hicho na kueleza kuwa wataendelea kutoa elimu bora kwa kuwajenga wanafunzi kitaaluma na nidhamu, leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wazazi wakichangia mada katika kikao hicho. Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani yao ya taifa ya kidato cha pili wakipokea zawadi na vyeti vya pongezi kutoka kwa uongozi wa shule hizo.
*****************
* Yafuta adhabu ya viboko baada ya nidhamu kuimarika zaidi
SHULE za St. Mary’s zimeeleza kufurahishwa na ukuaji wa nidhamu kwa wanafunzi wake hali iliyopekea kukuwa kwa taaluma kupitia matokeo ya mitihani mbalimbali ya kitaifa ikiwemo kidato cha pili na kidato cha nne.
Akizungumza mara baada ya kikao cha wazazi wa wanafunzi wa shule ya St. Mary’s tawi la Mbezi Beach Makamu Mkuu wa shule hiyo Rajab Balele amesema ushirikiano wa walimu na wazazi umeleta matokeo chanya ya ukuaji wa taasisi hiyo inayotoa huduma ya elimu.
Amesema kuwa, katika kikao hicho wamejadili juu ya malezi ya watoto kwa kuzingatia maadili ya kiafrika bila kupotosha na kuwakwamisha kufanya vizuri katika masomo yao.
“Pia tumejadili suala za wazazi kuwaleta wanafunzi kukaa bweni ili waweze kutumia muda mwingi katika masomo na hiyo ni pamoja na ufuatiliaji kwa wanafunzi katika masomo yao kwa kushiriki vikao vya wazazi na kuhakikisha wanafuatilia usalama wa wanafunzi pindi wanapofunga na kufungua shule na sio kutuma wawakilishi au kutuma madereva.” Amesema.
Amesema, baada ya kuimarika kwa nidhamu wameondoa adhabu ya viboko na kuwataka wazazi kuendelea kutoa ushirikiano zaidi ili kuboresha sekta ya elimu.
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo Ntipoo Recka amesema matokeo bora kumetokana na kujituma kwa walimu na ushirikiano bora kutoka kwa wazazi na nidhamu ya wanafunzi.
Ntipoo amesema wamefikia kiwango cha nidhamu kwa asilimia 99 na kuwataka wazazi kuwa mabalozi bora kupitia matokeo bora yanazidi kuimarika kila mwaka kwa shule hizo.
Hafla hiyo imekwenda sambamba na utoaji zawadi kwa wanafunzi wa kidato cha pili waliopata ufaulu ya daraja A kwa masomo 11 katika mitihani yao ya taifa.