Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Said Yakubu (kushoto) akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea programu hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali wanazozifanya.
Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika, Boniface Kadili (kulia) akitoa ufafanuzi wa matukio mbalimbali ya picha za harakati wa ukombozi waAfrika kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Said Yakubu wakati alipotembelea programu hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali wanazozifanya mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika, Boniface Kadili (kushoto) akitoa historia ya Programu hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Said Yakubu wakati alipotembelea programu hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali wanazozifanya mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Said Yakubu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mikakati mbalimbali ya kuitangaza Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika wakati alipotembelea programu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Said Yakubu (katikati) akizungumza na watumishi wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika wakati alipotembelea programu hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali wanazozifanya mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Said Yakubu (kushoto) akicheza mchezo wa bao lilotumika wakati wa harakati za Ukombozi wa Afrika mapema hii leo jijini Dar es Salaam alipotembelea Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika ,kulia ni Mratibu wa Programu hiyo, Bw. Boniface Kadili.
Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika, Boniface Kadili (kulia) akitoa taarifa ya maendeleo ya ukarabati wa jengo lilotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Said Yakubu wakati alipotembelea programu hiyo ili kujionea shughuli mbalimbali wanazozifanya mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………….
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Said Yakubu amefanya ziara yake ya kwanza kwenye Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika mapema hii leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na programu hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa habari na watendaji wa programu hiyo, Naibu Katibu Mkuu Bw. Yakubu amewataka kuhamasisha jamii juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na programu hiyo ikiwa ni pamoja na kuhifadhi na kuenzi urithi huo.
“Lengo la Programi hii ni kuhakikisha kuwa urithi wa ukombozi wa Afrika unatambuliwa, unahifadhiwa, unalindwa na kutangazwa nan chi wananachama wa Umoja wa Afrika,” alisema Naibu Katibu Mkuu, Bw. Yakubu.
Katika kuhamasisha Umma Naibu Katibu Mkuu aesema kuwa Serikali imeingia makubaliano ya awali na Shirika la Utangazaji nchini kupitia chaneli ya Safari ili kuandaa na kurusha vipindi mbalimbali vinavyohusiana na harakati za ukombozi wa Afrika na historia kwa ujumla.
“Pamoja na makubaliano yanayoendelea na Shirika la Utangazaji nchini (TBC) kupitia chaneli ya Safari, serikali inaendelea kuwahimiza wananchi hasa wanafunzi kutembelea programu hii na kujionea historia ya harakati za ukombozi wa Afrika,” alisema Naibu Katibu Mkuu, Bw. Yakubu.
Nae Mratibu wa Programu hiyo, Bw. Boniphace Kadili, amesema kuwa lengo la programu hiyo ni pamoja na kuratibu tafiti na kutangaza taarifa za urithi wa ukombozi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
“Pamoja na kuratibu tafiti mbalimbali, programu ina mpang wa kuendeleza utalii wa kiukombozi nchini kwa kushirikiana na wadau na mamlaka yenye dhamana ya utalii,” alisema Mratibu wa Programu Bw. Kadili.
Lengo la Programu hii ni kuendeleza ushirikiano na wadau pamoja nan chi wanachama wa programu hii kwa kusimamia na kuendelezaurithi wa ukombozi wa Afrika.