Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisikiliza maelezo ya Naibu Balozi wa Ireland nchini mhe. Bronagh Carr walipofanya mazungumzo ofisini kwake katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Naibu Balozi wa Ireland nchini Mhe. Bronagh Carr alipowasili ofisini kwake kwa ajili ya mazugumzo na Asasi ya Utawala wa Sheria ya ireland yaliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisikiliza maelezo ya wageni wake walipokutana ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na ugeni wa Asasi ya Utawala wa Sheria ya Ireland uliomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa na Mhe. Jaji Ailleen Donolley wa Mahakama Kuu ya Irelandambaye amekuja nchini na Asasi ya Utawala wa Sheria ya Ireland uliomtembelea mhe. Waziri ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa na Mhe. Jaji Ailleen Donolley wa Mahakama Kuu ya Ireland na Mary Rose Gearty Mwendesha Mashtaka nchini Ireland ambao wamekuja nchini na Asasi ya Utawala wa Sheria ya Ireland uliomtembelea mhe. Waziri ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.
*************
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Augustine Mahiga amekutana na asasi
isiyo ya kiserikali ya Utawala wa Sheria ya nchini Ireland ofisini kwake katika mji wa Serikali Mtumba ulioko Jijini Dodoma.
Ugeni huo ambao uliongozwa na Naibu Balozi wa Ireland nchini Bi. Brognagh
Carr ulijumuisha Jaji Ailleen Donolley wa Mahakama Kuu ya Ireland, Mary Rose
Gearty Mwendesha Mashtaka nchini Ireland, Kate Mulkerrins Mkuu wa Idara ya
Sheria katika Jeshi la Polisi nchini Ireland. Ugeni huo pia uliambatana na
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake katika Sheria na Maendeleo
Afrika tawi la Tanzania (WiLDAF) Anna Kulaya.
Katika mazungumzo yao wamezungumzia namna ya kuangalia jinsi ambavyo
wanaweza kutumia ujuzi na utaalamu wao katika kusaidia Mahakama nchini,
kuona vyanzo vya matatizo ya kijamii nchini na jinsi ya kusaidia kukakabiliana
navyo na kwa pamoja kuja na mpango wa kukabiliana na matukio ya ukatili wa
kijinsia nchini.
Ujumbe huo pua umejadili maeneo ambayo pande hizo mbii zinaweza
kushirikiana katika harakati za kukabiliana na vitendo cya ukatili wa kijinsia na
upatikanaji wa haki za kijinsia nchini.
Asasi ya Utawala wa Sheria inaundwa na wanasheria wa nchini Ireland inafanya
kazi ya kukuza utawala wa sheria katika nchi zinazoendelea kwa kutumia ujuzi
na wanasheria wa nchi hiyo kuhakikisha upatikanaji haki duniani na kuwezesha
wananchi kuishi katika jamii ambazo hazikabiliwi na matatizo ya kutokuwa na
usawa, rushwa na migogoro