Vinara wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara timu ya Yanga imetinga hatua ya robo fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuichapa mabao 2-1 Biashara United Mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mabao mawili katika kipindi cha kwanza yalitosha kabisa kuipeleka Yanga hatua hiyo ya Robo Fainali Yanga walipata bao la kwanza dakika ya 21 kupita kwa kiungo Mkabaji Yanick Bangala baada ya Yanga kuweka kambi katika goli la Biashara.
Bao la pili na la ushindi limefungwa na Mshambuliaji wao hatari dakika 28 Fiston Mayele akipokea pasi safi kutoka Saido Ntibazonkiza na bao la kufutia machozi la Biashara limefungwa dakika ya 37 Collins Opare.
Kwa Matokeo hayo Yanga inaungana na timu za Kagera Sugar,Coastal Union,Geita Gold,Azam FC pamoja na Tanzania Polisi huku sikisubiriwa timu mbili kuungana kwenye Robo Fainali.
Michuano hiyo inatarajia kukamilika kesho kwa mechi mbili Wakilishi katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Simba watacheza na Ruvu Shooting majira ya saa moja usiku uwanja wa Mkapa huku Pamba FC watakuwa nyumbani kucheza na Dodoma jiji katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.