Mhe. Mchengerwa akitambulishwa na kamati ya maandali ya tamasha la Sauti za Busara ili aongee na umati wa watu walioshiriki kwenye kilele cha tamasha hilo usiku wa kuamkia leo Februari 14, 2022 ZanzibarMhe. Mchengerwa akiongea na umati wa wageni walioshiriki kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara Februari 13, 2022 ZanzibarWaziri Mchengerwa akiteta jambo na Katibu Mkuu wake Dkt.Hassan Abbasi mara baada ya kuwasili kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara, huko Zanzibar Februari 13, 2022. Umati wa watu waliohudhuria kwenye kilele cha tamasha la Sauti za Busara Februari 13, 2022 huko Zanzibar.
Wasanii mbalimbali wakitumbuiza kwenye kilele cha tamasha la Sauti za Busara huko Zanzibar, Februari 13, 2022
**************************
Na. John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewakaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria tamasha kubwa la kimataifa la Sauti za Busara kutoka sehemu mbalimbali duniani kushiriki kwenye tamasha la kihistoria la muziki la Serengeti litakali fikia kilele chake Machi 12, mwaka huu jijini Dodoma.
Akizungumza kwenye kilele cha Tamasha la Sauti za Busara usiku wa kuamkia leo Februari 14, 2022 huko zanzibar amesema Serikali inakwenda kuandaa matamasha makubwa ya kihistoria ambayo yataonesha utamaduni wa kitanzania, hivyo dunia inakaribishwa kushuhudia tukio hili la kihistoria na kimataifa.
“Naomba kutumia nafasi hii kuwakaribisha kwenye Tamasha la Serengeti na Tamasha la kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo ambayo yanakwenda kuionyesha dunia utajiri wa utamaduni na vivutio vya utalii duniani”. Ameongeza Mhe. Mchengerwa.
Mhe. Mchengerwa pia aliambatana na Katibu Mkuu wake, Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi wa Sanaa . Dkt. Emmanuel Ishengoma.
Amepongeza Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo kwa kuandaa Tamasha hilo kwa kiwango cha kimataifa na kusisitiza kuwa Serikali itashirikiana nao ili kuhakikisha tamasha lijalo linafanyika.