Mbunge wa viti maalum (CHADEMA) Ester Matiko akiteta jambo na Mwenyekiti wa MISA TAN Bi.Salome Kitomari |
Normal
0
false
false
false
EN-US
X-NONE
X-NONE
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:8.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:107%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,sans-serif;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}
??MWANDISHI WETU
BAADHI ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wamezishauri taasisi za kihabari kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi
wa Habari nchini ili kuwajengea uwezo ili waweze kufanya kazi kwa weledi.
Wakichangia katika mjadala baada ya mafunzo ya
kuwajengea uwezo wa sheria mbalimbali za Habari yaliyofanyika mwishoni mwa wiki
jijini Dodoma yaliyoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika
tawi la Tanzania (MISA TANZANIA),wabunge hao wameoneshwa kutoridhishwa na maendelo
ya tasnia ya Habari katika siku za karibuni.
Wakizungumza kwa kutoa mifano ya baadhi ya Habari zinazoandikwa
katika vyombo mbalimbali vya Habari nchini kuhusu suala linalofukuta la hifadhi
ya Ngorongoro baadhi ya wabunge hao walisema tasnia ya Habari haijatenda haki
kujulisha umma undani wa suala.
Mbunge wa Viti Maalum (C
HADEMA) Esta Bulaya alibainisha
kwamba kuna kizazi cha waandishi wa habari mahiri kinapotea lakini hakuna
jitahada ya maksudi za kulea na kuibua waandishi wengine watakaofanya kazi za
kusisimua na kuibua mijadala mbalimbali kwa manufaa ya nchi.
Kuna kizazi kinapotea,waandishi tulionao hivi sasa
tunahitaji kuweka nguvu za ziada kwao ili wawe mahiri.,Wapo baadhi yao hawajui
hata kuuliza maswali,anapokufuata anakuwekea ‘mic’ anakwambia mheshimiwa we ongea
chochote tu kuhusu huu mjadala.
Ester Bulaya
Bulaya ameongeza kuwa mafunzo ya mara kwa mara
yatawasaidia waandishi hao kujijenga n ahata kuongeza uwezo wao wa kuuliza
maswali hivyo aliwataka MISA na Wadau wengine wa Habari kuwekeza nguvu katika
hilo.
Naye mbunge wa Momba(CCM),Condester Sichwale aliwataka
waandishi wa Habari kuandika Habari kwa weledi ili kuaminika katika jamii,na
pia ameshauri vyombo vya Habari kujikita katika kutafuta suluhisho kwa matatizo
ya yanayokabili jamii.
Tunaomba mjitahidi kusimamia maadili na miongozo
inayosimamia tasnia yenu,kuna baadhi ya mambo yanakuzwa na vyombo vya habari bila
sababu ya msingi na wakati mwingine Habari hizo zinaenda kupotosha jamii
Condester Sichwale
Mwenyekiti wa wabunge hao katika warsha hiyo Mbunge wa
Rashidi Shangazi alisema kuna haja Tanzania kuanzishwa baraza la walaji wa Habari
ili wao kama watumiaji wa Habari wawe na jukwaa la kufikisha maoni yao kuhusu
muenendo wa tasnia hiyo.
“Kama walaji wengine wana mabaraza yao na sisi walaji
wa Habari ni bora tukafikiria kuanzisha jukwaa letu ili inapobidi tuwaambie
kwamba mnachotulisha siyo tunachohitaji.”alisisitiza Shangazi.
Shangazi pia aliishukuru MISA TAN kwa kuwajengea uwezo
kundi hilo la wabunge na kuwashauri kuendelea na semina hizo kwa kamati
mbalimbali za bunge ili kuwaonesha namna baadhi ya vifungu vya sheria
zinazopitishwa bungeni zinavyaathiri uhuru wa tasnia ya Habari nchini.
Awali akifungua warsha hiyo mwenyekiti wa MISA TANZANIA Bi.Salome Kitomari alisema dhumuni kubwa la warsha hiyo ni kuwashirikisha wabunge hao mambo mbalimbali ambayo yapo katika sheria za Habari na yanachangia kudidimiza uhuru wa kujieleza.
“Tumewaita baadhi ya Wabunge wetu vinara kuwashirikisha kile ambacho waandishi wamekuwa wanakilalamikia mara kwa mara hivyo panapotokea mapitio ya sheria wawe na uzoefu na waweze kuona madhara ya baadhi ya vifungu vya sheria katika tasnia ya Habari.” Amesema Kitomari