Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kifedha ya Faidika (Faidika Microfinance Tanzania) Baraka Munisi akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kisasa wa kidigitali ijulikanao kwa jina la LetsGo Digital Mall ambapo unamwezesha mteja wao kupata huduma kwa kutumia simu ya mkononi, kupitia USSD namba *149*06#, mitandao na ‘App’ ya LetsGo powered by Letshego.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi aliyemwakilisha Waziri Dk Mwigulu Nchemba akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kisasa wa kidigitali ijulikanao kwa jina la LetsGo Digital Mall ambapo unamwezesha mteja wao kupata huduma kwa kutumia simu ya mkononi, kupitia USSD namba *149*06#, mitandao na ‘App’ ya LetsGo powered by Letshego.
Mwenyekiti wa bodi ya Taasisi ya Kifedha ya Faidika (Faidika Microfinance Tanzania) Adam Mayingu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kisasa wa kidigitali ijulikanao kwa jina la LetsGo Digital Mall ambapo unamwezesha mteja wao kupata huduma kwa kutumia simu ya mkononi, kupitia USSD namba *149*06#, mitandao na ‘App’ ya LetsGo powered by Letshego.
Fredrick Mmelesi ambaye ni Afisa Mkuu wa Ushirikiano na Maendeleo wa Letshego Africa wakishiriki akizungumza katika uzinduzi wa mfumo wa kisasa wa kidigitali ijulikanao kwa jina la LetsGo Digital Mall ambapo unamwezesha mteja wao kupata huduma kwa kutumia simu ya mkononi, kupitia USSD namba *149*06#, mitandao na ‘App’ ya LetsGo powered by Letshego.
Kutoka kushoto Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi ya Kifedha ya Faidika (Faidika Microfinance Tanzania) Adam Mayingu, Mkurugenzi Mkuu Baraka Munisi, Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi na Fredrick Mmelesi ambaye ni Afisa Mkuu wa Ushirikiano na Maendeleo wa Letshego Africa wakishiriki katika uzinduzi wa mfumo wa kisasa wa kidigitali ijulikanao kwa jina la LetsGo Digital Mall ambapo unamwezesha mteja wao kupata huduma kwa kutumia simu ya mkononi, kupitia USSD namba *149*06#, mitandao na ‘App’ ya LetsGo powered by Letshego.
*************************
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Wateja wa Taasisi ya kifedha ya Faidika wameboreshewa huduma, baada ya kuzinduliwa mfumo wa kisasa wa kidigitali ijulikanao kwa jina la LetsGo Digital Mall.
Mkurugenzi Mkuu wa Faidika Microfinance Tanzania, Bw Baraka Munisi alisema kuwa, wamefikia hatua hiyo ili kumwezesha mteja wao kupata huduma bora kwa njia rahisi na haraka zaidi.
Bw Munisi alisema kuwa kupitia LetsGo Digital Mall, mteja anaweza kupata mkopo mpya, kuongeza mkopo, taarifa za akaunti na huduma nyinginezo kwa njia ya simu ya mkononi kupitia USSD namba *149*06#, mitandao na ‘App’ ya LetsGo powered by Letshego.
Kwa mujibu wa Bw Munisi, huduma ya LetsGO Digital Mall itatumika kama kichocheo cha kuwafikia wateja wengi ili kupata huduma za kisasa bila kutembelea ofisi zao.
“LetsGo Digital Mall ni jukwaa linalozingatia wateja na lenye kurahisisha mtumiaji kupata huduma mbalimbali kwa wakati muafaka bila ya usumbufu wowote.
Kupitia LetsGO Digital Mall, wateja wetu watapata huduma bora zaidi za kifedha kwa kuzingatia falsafa ya LetsGO Nation bila ya usumbufu wowote katika wakati na eneo muafaka,” alisema Bw Munisi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Faidika Microfinance Tanzania Bw Adam Mayingu alisema kuwa huduma hiyo ni jukwaa bora kwa sasa na wakati ujao hasa kwa njia ya kidigitali.
Bw Mayingu alisema kuwa wametumia teknolojia ya hali ya juu ili kufanikisha huduma hiyo na lengo kuu ni kuwanufaisha na kuwaondolea wateja wao usumbufu.
Alifafanua kuwa huduma yao ya kigitali inadhihirisha jinsi gani walivyokuwa mstari wa mbele katika kuwajali wateja wao katika huduma za kifedha.
“Tunajisikia fahari kubwa kuwekeza shughuli zetu kwa Watanzania na kuwapa huduma bora kwa njia ya kidigitali zaidi,” alisema Bw Mayingu.
Alifafanua kuwa uwekezaji wa kidigitali unasaidia kuongeza viwango vya huduma bora katika huduma mbalimbali.
“LetsGo” ni huduma mpya katika katika taasisi yetu yenye lengo la kuleta mageuzi ya huduma za kidigitali hapa nchini na kimataifa,” alisema.
Alisema kuwa ni fursa kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kutumia huduma hii mpya ili kufikia malengo yao.
“FaidikaMicrofinance inawaalika watu wote kujiunga na huduma ya LetsGoNation yenye lengo la kuleta mapinduzi ya kidigitali kwa Waafrika wenye lengo la kusaidia kukua kwa uchumi,” aliongeza.