Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi akitoa taarifa katika Kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kilichoketi wilayani humo. mkoani Singida leo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga akizungumza kwenye baraza hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Peter Mtyana akitoa taarifa katika baraza hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Justice Kijazi (kulia) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally Mwanga kwenye baraza hilo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa akizungumza kwenye kikao hicho.
Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Singida, Adamu Kilongozi akitoa mada kwa madiwani hao kuhusu posho wanazostahili kulipwa.
Mratibu wa baraza hilo la Madiwani wilayani humo, Peter Bahati akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhandisi Paskas Mulagiri akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii wa Halmashauri hiyo Selestine Yunde akichangia jambo kwenye baraza hilo.
Madiwani Leonard Muna wa Kata ya Iseke (kushoto) na Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Ihanja, Mariam Ntembo wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Diwani wa Kata ya Ihanja Mohamed Igae (kulia) na Abel Suri wa Kata ya Unyahati wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Diwani wa Kata ya Mwaru, Iddi Makangale na Deogratius Majige (kulia) wa Kata ya Mgungira wakiwa kwenye baraza hilo.
Baraza likiendelea.
Baadhi ya maafisa watendaji na wataalamu wa halmashauri hiyo wakiwa kwenye baraza hilo
Afisa Mtendaji wa Kata ya Dung’unyi, Yahaya Njiku (kushoto mbele) akiwa na watendaji wenzake kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Diwani wa Kata ya Mungaa Dulle Gabriel akichangia jambo kwenye baraza hilo.
Diwani wa Kata ya Unyahati Abel Suri akizungumza kwenye baraza hilo.
Baraza likiendelea.
Diwani wa Kata ya Mang’onyi, Innocent Makomelo akizungumza kwenye baraza hilo.
Diwani wa Kata ya Mtunduru Ramadhan Mpaki akichangia jambo.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Diwani pekee kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika halmashauri hiyo wa Kata ya Ntuntu, Athumani Toto akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Issuna Stephen Misai (kushoto) na Diwani wa Kata ya Iglanson Yusuph Athuman yakipitia makabrasha kwenye kikao hicho.
Madwani wa Viti Maalumu wakiwa kwenye kikao hicho.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Abubakar Muna akipitia kabrasha katika kikao hicho.
Zawadi kwa watendaji waliokuwa vinara wa kukusanya mapato ya halmashauri hiyo wakikabidhiwa zawadi.
Zawadi zikitolewa kwa wakusanya mapato wazuri.
Zawadi kwa watendaji waliokuwa vinara wa kukusanya mapato ya halmashauri hiyo wakikabidhiwa zawadi.
Mratibu wa Anuani za Makazi Wilaya ya Ikungi, Joan Katanga akizungumzia zoezi la Anuani za makazi.
Madiwani wa Viti Maalumu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Helena Petro (kulia) na Theresia Masinjisa kutoka Kata ya Mtunduru wakiwa kwenye kikao hicho.
Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Makiungu, Zainabu Ntui (kushoto) na Diwani wa Kata ya Lighwa Gabriel Mukhandi wakiwa kwenye kikao hicho.
Na Dotto Mwaibale, Singida
HALMASHAURI ya Wilaya ya Ikungi hadi kufikia Desemba 30, 2021 imepokea Sh.1,851,383,325 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika kipindi cha 2021/2022 imefahamika.
Kati ya fedha hizo Sh.1,732,271,325 sawa na asilimia 16 ni fedha za Ruzuku kutoka Serikali Kuu na Sh.119,109,000 sawa na asilimia 17 ni fedha za mapato ya ndani na fedha zilizopokelewa kutoka nje ya bajeti ni takribani Sh.4,708,496,326.02. Bilioni.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Justice Kijazi wakati akitoa taarifa kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani kilichoketi leo wilayani humo.
Kijazi alisema katika kipindi hicho halmashauri hiyo iliidhinishiwa kutumia jumla ya Sh.10,557,336,409 za miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu, Wahisani na Sh.680,000,000 kutoka mapato ya ndani.
Akitoa mchanganua wa matumizi ya fedha hizo alitaja mradi wa kwanza kutekelezwa kuwa ni ujenzi wa madarasa sita ya Shule ya Msingi Gelmany ambao utatumia Sh.125 Milioni na kuwa mchakato wa ujenzi huo unaendelea, ujenzi wa madarasa na vyoo Shule ya Msingi Kimbu fedha zilizotolewa ni Sh.93 Milioni, Mradi wa miundombinu ya maji na vyoo Shule ya Msingi Ighuka, Mnyanghe na Iglanson Sh.165 Milioni.
Alitaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Matale, Ilolo na Mtunduru Sh. 260 Milioni, ujenzi wa madarasa 65 pamoja na madawati katika shule Shikizi ni Sh.1.3 Bilioni, ujenzi wa shule za sekondari Makilawa na Matondo Sh. 940 Milioni, ujenzi wa jengo la utawala Shule ya Sekondari ya Issuna na maji- Ndagu Sh. 80 Milioni, ujenzi wa madarasa 67 ya shule za sekondari Sh.1.3 Bilioni, ujenzi wa madarasa nane shule za sekondari za Utaho, Dk. Shein, Ntuntu, Sepuka na Lighwa Sh.100 Milioni.
Kijazi alitaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Sh.800 Milioni,ujenzi wa zahanati nne, Ufana, Makotea, Kinyampembee na Usule Sh.200 Milioni, Ujenzi wa Kituo cha Afya Masutianga Sh.300 Milioni, ujenzi wa vyoo vya zahanati, Mkhuwi, Matongo,Dung’unyi na Ntuku Sh.88.9 Milioni, ujenzi wa vituo vya Afya Ntuntu na Iglanson Sh.500 Milioni, Uhamasishaji wa chanjo Sh.51 Milioni, ujenzi wa nyumba ya Mganga Hospitali ya wilaya Sh.90 Milioni.
Aidha Kijazi alisema halmashauri hiyo imepokea fedha za mkopo Sh.500.9 kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kutengeneza mji wa kisasa na kuwa mchakato wa kazi hiyo unaendelea.
Kijazi alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa halmashauri hiyo kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo na akawapongeza watendaji wote pamoja na madiwani kwa ushiriano walionao kwa kuiwezesha halmashauri hiyo kwa miaka sita mfululizo kupata hati safi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga alisema wamepokea zaidi ya Sh. 4.1 Bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo hivyo alimuomba mkurugenzi wa Justice Kijazi pamoja na timu yake kuhakikisha fedha hizo zinaenda kufanya kazi iliyokusudiwa na si vinginevyo.
“Nawaombeni madiwani nendeni mkasimaie matumizi ya fedha hizo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwani kazi hii inahitaji ushirikiano wa kila mmoja wetu” alisema Mwanga.
Mwanga aliwaomba madiwani hao kwenda kuisimamia miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na viwango vinavyokubalika huku thamani yake ikilingana na fedha zilizotolewa.
Awali akitoa mada kwa madiwani hao Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Singida, Adamu Kilongozi aliwatahadharisha madiwani hao kuwa wahangalifu na kujiepusha kupokea fedha (posho) wasizojua chanzo chake ili wasijekujikuta wakiwa kwenye migogoro baina yao na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) au mikononi mwa polisi huku wakitoa visingizio kuwa walikuwa hawajui chochote.
Kilongozi akitoa mmoja wa mfano kati ya mingi aliyoitoa alisema ni kosa kwa diwani au mtumishi yeyote wa Serikali ambaye amepewa usafiri (gari) kwenda kufanya kazi sehemu fulani na baada ya kumaliza kazi hiyo kupewa posho ya usafiri.
Alisema jambo hilo halikubaliki na mtumishi wa namna hiyo anaweza kujikuta akiangukia kwenye kosa la rushwa na kuchukuliwa hatua.
Aidha Kilongozi aliongeza kuwa diwani au mkuu wa idara anapotekeleza wajibu wake hawezi kusaini posho ya siku tanoili hali akijua siku halizotumia nje ya eneo lake la utawala au kazi zilikuwa pungufu na akibainika kufanya hivyo atakuwa ametenda kosa kisheria.