***********************
Na. John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa kesho Februari 12, 2022 ataanza kufanya dhukuru na wadau wa sekta ya Filamu jijini Dar es Salaam ikiwa ni mkakati wa makusudi wa kufanya tafakuri ya pamoja na wadau mbalimbali wa sekta anazoziongoza ili kutatua changamoto zinazowakabili na kuleta mapinduzi ya haraka.
Haya yameelezwa leo Februari 11, 2022 na Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi wakati akizindua rasmi Tamasha la Muziki la Serengeti jijini Dar es Salaam.
Amesema kundi la kwanza analokutana nalo kesho litahusisha wadau mbalimbali wa filamu ambao ni pamoja na watayarisha,waongozaji, wapiga picha, waandika miswada, waigizaji, wahariri na walimu kutoka shirikisho la filamu.
Akizungumza alipotembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) hivi karibuni Mhe. Mchengerwa amelielekeza TaSUBa na wadau mbalimbali wakiwemo wazalishaji wa muziki hapa nchini kuandaa muziki wa kitanzania ambao utalitambulisha taifa la Tanzania duniani.
Aidha, katika hotuba yake ya kwanza kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za muziki alisisitiza kuwa Wizara yake inakwenda kufungua milango kwa wadau mbalimbali wa sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kujadili kwa pamoja changamozo wanazokabiliana nazo na kulimaliza katika kipindi kifupi.”
Sisi kama Wizara yenye dhamana ya utamaduni, Sanaa na michezo tunawaahidi wadau wetu kuwa karibu naoi li kuleta mapinduzi makubwa kwenye maeneo hayo hivyo nawaomba watumishi kufanya kazi kwa kasi na weledi wa hali ya juu, sitamvumilia mtumkishi yoyote, mvivu na mzembe.” Alisisitiza Mhe. Mchengerwa.
Aidha kikao cha kesho ni ahadi aliyoitoa Mhe. Mchengerwa ya kukutana na wasanii wa makundi yote katika kipindi kifupi kijacho ili kujua changamoto zinazowakabili kwenye kazi zao ili kupata ufumbuzi wa pamoja.