************************
Kuna barua pepe feki inayosambaa mitandaoni kuhusu kuwepo kwa mchakato wa ajira Benki Kuu wa kuchukua wafanyakazi kutoka Taasisi mbali mbali za Fedha. Taarifa hizi hazina ukweli wowote, hivyo zipuuzwe.
Barua pepe hiyo feki ya tarehe 5 Februari, 2022 yenye kichwa cha habari “OMBI LA KUKUAJIRI BOT” ambayo inaonesha kutumwa kupitia barua pepe ya Benki Kuu ya [email protected] imemtaka aliyeandikiwa kuwasilisha maombi yake ya ajira kupitia barua pepe ya [email protected].
Aidha, taarifa hiyo feki inaonesha kuwepo kwa mawasiliano kati ya mtu aitwaye Irene Millinga ([email protected]) na mtu aitwaye Dr. Tefilo Richard ([email protected] ) tarehe 8 na 9 Februari, 2022 kupitia barua pepe yenye kichwa cha habari “MCHAKATO WA AJIRA BOT”.
Taarifa hizi zote ni za uongo. Bila shaka zimeandaliwa na watu wenye nia ovu ili kuwatapeli watu kwa imani kuwa watapata ajira Benki Kuu. Hakuna mchakato wowote wa ajira unaoendelea Benki Kuu kwa kuchukua wafanyakazi kutoka Taasisi mbali mbali za Fedha.
Hivyo, taarifa hizo zipuuzwe. Aidha, tunawaonya watu wanaojihusisha na kutunga taarifa za uongo za namna hii kuacha mara moja kuepuka hatua za kisheria dhidi yao.
Imetolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki [email protected]