Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tamasha la Muziki la Serengeti 2022. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 11/02/2022 katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tamasha la Muziki la Serengeti 2022. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 11/02/2022 katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam Msanii wa kizazi kipya Faridi kubanda (FID Q) akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tamasha la Muziki la Serengeti 2022. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 11/02/2022 katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi akiwa pamoja na msanii wa kizazi kipya Faridi kubanda (FID Q) wakionesha nembo ya Tamasha la Muziki la Serengeti la 2022 ambalo litafanyika mwezi Machi 2022.
******************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
TAMASHA la Muziki la Serengeti 2022 limerudi tena kwa mara nyingine ambapo leo hii limezinduliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas.
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Dkt.Abbas amesema Tamasha hilo litakuwa bora na la kihistorra kwani takribani wasanii 50 watatumuiza katika tamsha hilo ambalo litafanyika Mwezi Machi 2022 Jijini Dodoma.
Amesema Tamasha hilo linakusudiwa kutangaza utamaduni na vivutio mbalimbali vinavyopatikana hapa nchini.
“Wananchi mjitokeze kwa wingi, hamtajutia kushiriki kwa maana kutakuwa matukio mbalimbali ambayo yatafanyika siku hiyo, ambayo yatakuwa mazuri na kuweza kuburudika ipasavyo”. Amesema Dkt.Abbas.
Aidha Dkt.Abbas amesema wasanii wakongwe na wachanga watashiriki ili kuleta ladha tofauti tofauti kwenye Tamasha hilo, na watakaopewa fursa ya kutoa burudani watatumia fursa hiyo vizuri kuonesha vipaji vyao na kutoa burudani ya kutosha kwa mashabiki wa muziki nchini.
Kwa upande wake msanii wa Muziki wa kizazi kipya Farid Kubanda (FID Q) ameishukuru Wizara kwa kuandaa matamasha ya muziki nchini kwani yanajenga na kutoa fursa kwa wasanii ambao wamekuwa hawaonekani kwa urahisi kuonesha vipaji vyao.