Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Bahati Geuzye akisaini Makubaliano Maalum ya kushirikiana na Shirika la BRAC – Maendeleo Tanzania kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Bahati Geuzye (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la BRAC – Maendeleo Tanzania Bi. Susan Bipa wakisaini makubaliano maalum kwa ajili ya kusaidia kuboresha miundombinu ya elimu katika jiji la Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Bahati Geuzye (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la BRAC – Maendeleo Tanzania Bi. Susan Bipa wakionesha wajumbe wa Menejimenti ya TEA (hawapo pichani) makubaliano maalum waliosaini kwa ajili ya kusaidia kuboresha miundombinu ya elimu katika jiji la Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Bahati Geuzye (wa pili kushoto) akipokea moja ya Kompyuta mpakato zitakazopelekwa kwenye baadhi ya shule za jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la BRAC – Maendeleo Tanzania Bi. Susan Bipa (kushoto). Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa miradi kutoka TEA Bi. Anna Makundi pamoja na Mkurugenzi wa huduma za Taasisi TEA, Dkt. Erasmus Kipesha.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Bahati Geuzye (wa pili kushoto) akipokea moja ya Kishikwambi (Tablet) zitakazopelekwa kwenye baadhi ya shule za jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la BRAC – Maendeleo Tanzania Bi. Susan Bipa (kushoto). Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa miradi kutoka TEA Bi. Anna Makundi pamoja na Mkurugenzi wa huduma za Taasisi TEA, Dkt. Erasmus Kipesha.
***********************
Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wameingia mkataba wa makubaliano na Shirika lislo la Kiserikali la Brac- Maendeleo Tanzania kushirikiana katika utekelezaji wa miradi inayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za TEA leo Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bi. Bahati I. Geuzye amesema kupitia makubaliano hayo yatachangia kusukuma mbele jitihada za nchi yetu katika kufikia lengo namba nne la Maendeleo Endelevu ya Millenia linalohimiza elimu bora, yenye usawa na kutoa fursa kwa wote kujiendeleza.
Amesema kupitia makubaliano hayo, katika mwaka wa kwanza BRAC – Maendeleo Tanzania, imepanga kutoa Kompyuta 120 ambazo zinajumuisha Kompyuta Mpakato 60 na Vishikwambi (Tablets) 60 zikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 132.6.
“Kompyuta hizi zitapelekwa katika shule tatu (3) za Sekondari katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam ambazo ni Miburani, Wailes na Karibuni. Shule nufaika zitakuwa na vyumba maalum vya kompyuta (Computer Lab) vitakavyotoa fursa ya wanafunzi kujifunza kwa vitendo elimu ya Kompyuta. Msaada huu utanufaisha wanafunzi 600 na walimu 26 katika shule hizo”. Amesema Bi.Geuzye.
Aidha amesema BRAC – Maendeleo Tanzania imedhamiria kutoa msaada huuo kwa miaka mitatu mfululizo hivyo matarajio yetu ni kuwa hadi msaada huu unakamilika jumla ya Kompyuta 360 zitakuwa zimetolewa, wanafunzi 1800 na walimu 78 watakuwa wamenufaika.
Pamoja na hayo Bi.Geuzye ametoa rai kwa shule zitakazonufaika na msaada huo wa Kompyuta kuzitumia na kuzitunza vizuri ili zidumu na kunufaisha kundi kubwa la wanafunzi.