NAIBU Waziri wa Afya, Dk.Godwin Mollel,akiwaongoza watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais,jiji,uongozi wa Soko pamoja na Wafanyabiashara wa soko leo Februari 10,2022 kufanya usafi wa mazingira katika Soko la Chang’ombe na kutoa elimu ya utenganishaji wa taka, mifuko na vifungashio vya plastiki ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga,akifanya usafi wa mazingira katika Soko la Chang’ombe na kutoa elimu ya utenganishaji wa taka, mifuko na vifungashio vya plastiki ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Dk. Andrew Komba,akifanya usafi wa mazingira katika Soko la Chang’ombe na kutoa elimu ya utenganishaji wa taka, mifuko na vifungashio vya plastiki ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Wafanyabiashara wa soko la Chang’ombe Dodoma wakifanya usafi wa mazingira katika Soko hilo leo Februari 10,2022 ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Afya, Dk.Godwin Mollel,akizungumza mara baada ya kushiriki zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika Soko la Chang’ombe na kutoa elimu ya utenganishaji wa taka, mifuko na vifungashio vya plastiki ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga,akizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika Soko la Chang’ombe na kutoa elimu ya utenganishaji wa taka, mifuko na vifungashio vya plastiki ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Abdallah Mahiya ,akielezea mikakati ya jiji hilo akizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika Soko la Chang’ombe na kutoa elimu ya utenganishaji wa taka, mifuko na vifungashio vya plastiki ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
Ofisa Mazingira wa Jiji la Dodoma,Ally Mfinanga,akielezea mikakati ya kuliweka jiji katika mazingira bora mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika Soko la Chang’ombe na kutoa elimu ya utenganishaji wa taka, mifuko na vifungashio vya plastiki ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
……………………………………………………………
Na.Alex Sonna,DODOMA
NAIBU Waziri wa Afya, Dk.Godwin Mollel amelitaka Jiji la Dodoma kuweka mkazo katika kuhamasisha wananchi kupanda miti badala ya kutoa maelekezo ya upakaji wa rangi kwenye mabati peke yake.
Dk.Mollel ameyasema hayo leo Februari 10,2022 wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika Soko la Chang’ombe na kutoa elimu ya utenganishaji wa taka, mifuko na vifungashio vya plastiki ikiwa na wiki ya uzinduzi wa sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021,inayotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango Februari 12,2022 jijini Dodoma.
“Moja ya sifa mtu kuja nje kwako akute mazingira safi yenye miti ya kuvutia, sasa nyie Dodoma mmetupangia rangi za mabati lakini hamjatupangia tuoteshaje miti, mmekomalia rangi za mabati kuliko uoteshaji miti,”amesema Dk.Mollel.
Aidha Dk.Mollel amewahimiza wazazi kuwapatia watoto wao miti ya kuotesha maeneo ya shule ili atunze.
Pia amewataka wananchi kuzingatia suala la usafi katika maeneo yao ili kuondokana na magonjwa ya kuambukiza yanayopelekea kutumia gharama kubwa kwa matibabu.
“Gharama ya kusafisha mazingira ni kidogo kuliko gharama ya wewe kwenda hospitali kujitibu magonjwa yanayotokana na mazingira chafu,”amesema
Hata hivyo Dk.Molle amewahimiza wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19 ili kujikinga na maambukizo ya ugonjwa huo.
Naye, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi.Mary Maganga amesema usafi huo ni mwendelezo wa shughuli ya wiki ya uzinduzi wa Sera hiyo itakayozinduliwa siku ya Jumamosi na Makamu wa Rais, Dk.Philip Mpango jijini Dodoma.
“Tumepanda miti maeneo mbalimbali Medeli, Iyumbu tukishirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu(TFS) na Jiji la Dodoma kufanya usafi kwenye barabara na soko, ”amesema Bi.Maganga
Kwa upande wake, Ofisa Mazingira wa Jiji hilo, Ally Mfinanga, amesema kuna umuhimu wa wananchi kutenganisha taka ikiwamo za plastiki ili kuipunguzia mzigo Halmashauri inayotumia asilimia kubwa ya fedha zake katika usafirishaji wa taka.
“Pia mabaki ya chakula yanasaidia kulisha mifugo, sisi tunasisitiza watu watenganishe taka kwa kuwa inasaidia Halmashauri kupunguza gharama kubwa za kudhibiti taka ngumu ambapo asilimia 70 ya fedha hutumika kusafirisha taka,”amesema Mfinanga