ya Jamii Dkt. Zainab Chaula kushoto akizungumza wakati wa kikao hicho wa kwanza kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu
kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira
Mbunge wa Viti Maalumu
kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira
Mbunge wa Viti Maalumu
kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira akisistiza jambo wakati wa kikao hicho
Mkutano ukiendelea
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maendeleo
ya Jamii Dkt. Zainab Chaula amekutana na Asasi za Kiraia AZAKI kutoka Mikoa
ya Dodoma, Singida na Iringa lengo likiwa kujadili juu ya Ustawi wa taasisi
hizo nchini
Mkutano huo ulifanyika ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma huu ni utekelezaji wa ombi la Mbunge wa Viti Maalumu
kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira kuhusu Wizara hiyo
kukutana na NGOs za Mikoani na ombi hili aliwasilisha alipokutana na Katibu
Mkuu huyo Januari 24 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Katibu
Mkuu Chaula amesema kikao hicho na mambo mengine kimelenga kupokea changamoto,
kutoa elimu ya namna ya kuendesha AZAKI kwa kufuata sheria, kanuni na
taratibu ikiwemo kukabiliana na namna ya kuimarisha sekta hiyo.
Ameongeza kuwa kikao hicho kimetoa
fursa kwa AZAKI kutoka mikoani kutoa maoni yao na kupata uwakilishi katika
vikao na wizara kutokana na kwamba Asasi hizo zimekuwa na mchango mkubwa
katika maendeleo ya Tanzania.
Ambapo zimekuwa zikitoa elimu kwa
wananchi kuhusu mipango mbalimbali ya Serikali ikiwemo mabadiliko ya Tabia ya
nchi, masuala ya kiafya na kidemokrasia.
Akizungumza wakati wa Kikao hicho
,Mbunge Neema Lugangira amesema lengo ni kutoa fursa kwa NGOs za mikoani
kutoa maoni yao na kupata uwakilishi katika vikao na Wizara
Alisema pia lengo lengine ni kupokea
changamoto, kutoa elimu ya namna ya kuendesha NGOs kwa kufuata sheria na
kanuni na taratibu na kukubaliana namna ya kuimarisha Sekta ya Azaki.