…………………………………………………….
Na Farida Said, Morogoro.
Uwepo wa mradi wa Mkaa endelevu unaosimamiwa na shirika la uhifadhi wa misitu ya Asilia Tanzania TFCG pamoja na mtandao wa jamii wa usimamizi wa misitu Tanzania MJUMITA katika Kijiji cha Chabima Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro umesaidi kwa kiasi kikubwa kuhifadhi, kulinda na kuwanufaisha wakazi wa Kijiji hicho.
Hayo yameelezwa na Wananchi wa Kijiji cha Chabima wakati wa ziara ya wajumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya Kilosa ambapo wameishukuru TFCG kwa mradi huo huku wakiomba serikali kuwasaidia uapatikana wa vifaa bora na vya kisasa vitakavyoweza kuwasidia katika shughuli ya uvunaji wa mazao ya misitu ikiwemo mkaa kwa njia endelevu, mbao pamoja na kuni.
“Tunaishukuru sana TFCG na MJUMITA kwa kutuletea mradi wa mkaa endelevu umetusaidia sana kukizi mahitaji yetu ya kila siku, kama mimi nimewezeza kununua Mbezi nimejenga Nyumba na kuingia kikoba kupitia MKAA ENDELEVU .”Alimsema Bi Berita Hussein Mkazi wa Chabima.
Akizungumza katika ziara hiyo katibu wa CCM Wilaya ya Kilosa Shaban Mdoe licha ya kuipongeza TFCG pamoja na MJUMITA kwa kazi nzuri walioifanya amewataka wanachi pamoja viongozi wengine kuendelea kutoa elimu hiyo ya uvunaji wa wa MKAA ENDELEVU hata mara baada ya mradi kumalizika.
Kwa upande wake Meneja Mradi wa kuhifadhi misitu kupitia biashara endelevu kwa mazao ya misitu Bwana Charles Leonad amesema kuwa kupitia mradi huo umesaidia misitu 35 iliyohifadhiwa na vijiji kutoka Wilaya za Kilosa, Mvomero na Halmashauri ya Morogoro kutambulika kidunia.
Aidha amesema kutambulika kwa misitu hiyo kutatoa fulsa kwa mataifa mbalimbali duniani kuwezesha shughuri za uhufadhi wa mazingira, huku ikitajwa kutoa mchango mkubwa kwa jamii zinazozunguka misitu hiyo kunufaika na miradi ya utunzaji misitu ya asili.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaji Majidi Mwanga amekemea tabia ya viongozi wa vijiji kuingilia majumu ya kamati za misitu hali inayochangia ongezeko kubwa la uharibifu wa misitu ya asili iliyotengwa na kuhifadhiwa na jamii.
Pia Alhaji Mwanga ameiasa jamii kujiepusha na vitendo vyote ambavyo vitakuwa sababu ya uharibifu wa misitu hiyo ambao imekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo kupitia MKAA ENDELEVU.
Mradi wa MKAA ENDELEVU unatekelezwa katika Mikoa mitatu ya Iringa, Morogoro na Lindi kupitia Wilaya saba za Liwale,Mvomero, Kilosa, Wilaya ya Morogoro, Kilolo,Nachikwea na Luangwa.