**********************
Rais mpya wa MasterCard International- Sub Sahara Africa, Mark Elliott, ameshuhudia droo ya wiki ya tano ya Kampeni ya NMB MastaBata, ambako washindi 100 wamejishindia jumla ya Sh. Mil 10, hivyo kufanya pesa zilizotolewa kwa washindi 525 kufikia Sh. Mil. 75 Kati ya zaidi ya Sh. Mil. 200 zinazoshindaniwa.
NMB MastaBata – Kivyako Vyako,’ ilianza mwishoni mwa Desemba 2021, ambako kila wiki washindi 100 hutafutwa kupitia droo zinazosimamia na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT). Washindi 25 wa droo ya mwisho wa mwezi hujishindia Sh. Mil. 1 kila mmoja, huku wana fainali 30 wakitarajiwa kujinyakulia Sh. Mil. 3 kila mmoja hapo Machi mwishoni.
MasterCard ni washirika wa kibiashara wa NMB, ambako mwaka jana 2021 Kampuni hiyo iliitunukia NMB Tuzo ya Benki Kinara Katika Kuhamasisha Matumizi ya Kadi, ambako Leo Rais Mark Elliot, ameshuhudia moja ya droo ya kampeni hio.
Akizungumza kabla ya droo, Meneja wa Idara ya Kadi NMB, Sophia Mwamwitwa, alisema tayari washindi 400 wa droo za kila wiki walishatwaa Sh. Mil. 40, huku washindi 25 wa droo ya mwisho wa mwezi Januari wakijinyakulia Sh. Mil. 25, hivyo kupatikana kwa washindi 100 wa droo ya 5, kuigawa kampeni hiyo nusu kwa nusu kuelekea ‘Grand Finale’ mwishoni mwa Machi mwaka huu.
Droo hiyo ilifanyika chini ya usimamizi wa Mkaguzi wa GBT, Joram Mtafya, ambaye aliwahakikishia wateja wa NMB kuwa, kampeni hiyo inaendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu zinazotambuliwa na bodi yake na kwamba uwepo wake hapo ni mfululizo wa utekelezaji wa majukumu yao ya kuhakikisha washindi wanapatikana kihalali, huku akiwatoa hofu wateja wote.