………………………………
Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini kimeadhimisha Miaka 45 tangu kuzaliwa kwake ambapo shughuli mbalim za kijamii zimefanyika ikiwemo upandaji wa miti ili kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko tabia nchi.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika kata ya Mwamalili iliyopo Manispaa ya Shinyanga ambapo chama hicho kimefanya shughuli mbalimbali katika kata zote ikiwemo usajili wa wanachama, uingizaji wa wananchama wapya kwa mfumo wa Tehama pamoja na shughuli za ujenzi wa ofisi za chama.
Katika Wilaya ya Shinyanga mjini maadhimisho hayo yalianza tangu Januari 23, Mwaka huu 2022 ambapo chama hicho kimepanda miti sehemu mbalimbali ikiwemo taasisi za serikali pamoja na ofisi za chama ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho kuelekea kilele chake Februari 05,Mwaka huu ambapo chama kitatimiza Miaka 45 tangu kuzaliwa kwake.
Akizungumza katibu wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Agnes Bashemu amewaomba wananchi pamoja na viongozi kuitunza miti ambayo imepandwa katika kipindi cha kuadhimisha miaka 45 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
Bashimu amewasisitiza wanachama wa chama hicho Wilaya ya Shinyanga mjini kuendelea kuopanda miti ili kukabiliana na mabadiliko tabia nchi ambapo amesema miti hiyo itasaidia kupata matunza, vimvuli na kupendezesha mazigira kwa mwonekano wa rangi ya kijani.
Katibu huyo wa Wilaya ya Shinyanga mjini Bashemu amesema Mwaka huu 2022 litafanyika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa nchi nzima ambapo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo ambalo ni muhumu.
“Tunawaomba wananchi wajitokeze maana imekuwepo tabia ya watu kutoshirikia zoezi la sensa wanaona ni kitu cha kawaida lakini tunaendelea kusisitiza kwa sababu mikutano yetu bado inaendelea kwamba muda utakapofika wananchi wajitokeze kuhesabia na ratiba itakapo toka sisi kama chama kila kila balozi atahakikisha kwenye shina lake watu wake wote wamehesabiwa”.
Bashemu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan huku akiwaomba wananchi wote kuendelea kuiamini serikali na viongozi wote waliyopo madarakani kwa kuunga mkono jitihada zote zinatotolewa kwa lengo la kuleta matokeo chanya.
Kwa upande wake mgeni rasmi akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kata ya Mwamalili mjumbe wa kamati ya siasa ya Mkoa wa Shinyanga Grace Samwel amewasisitiza wananchi kupendana, kushirikiana huku akiwakumbusha kuwa na utaratibu wa kuingia kwenye nyumba za ibada hasa siku husika.
Mjumbe huyo wa kamati ya siasa mkoa wa Shinyanga Grace amewaomba wanachama na viongozi mbalimbali wa chama kuhakikisha wanajenga ofisi za vyama hasa kwenye matawi.
Grace amewasisitiza wananchi kujitokeza kwenye uchaguzi mkuu wa ndani huku akiwataka viongozi wa matawi husika katika mbalimbali kuacha tabia za kuficha fomu.
Grace ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kwa kuboresha miundombinu katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Elimu na Afya.
Kwa upende wao baadhi ya wananchi ambao wamehudhuria katika maadhimisho hayo wamekishukuru chama cha mapinduzi CCM kwa kufanya shughuli mbalimbali katika kata hiyo ikiwemo upandaji wa miti katika Zahanati ya Mwamalili pamoja na Shule ya msingi Twendepamoja iliyopo kata ya Mwamalili.