Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) akikipongeza Chama cha watoa Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA) kwa kutoa maoni yao kuhusu vyanzo vipya vya kodi wakati wa Mkutano na wajumbe wa Chama hicho, jijini Dodoma, Kushoto ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nauye na Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) akikipongeza Chama cha watoa Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA) kwa kutoa maoni yao kuhusu vyanzo vipya vya kodi wakati wa Mkutano na wajumbe wa Chama hicho, jijini Dodoma, Kushoto ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nauye na Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali (Mb), akieleza jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) na Chama cha watoa Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA), jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu (Sera) wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru (kushoto) akifafanua jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani) na Chama cha watoa Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA), jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Japhet Justine, Kaimu Kamishina wa Idara ya Sera, Bw. William Mhoja na Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara hiyo, Dkt. John Sausi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom, Bw. Sitho Mdlalose, akiongea kwa niaba ya wajumbe wa Chama cha watoa Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA) kuhusu mapendekezo ya vyanzo vipya vya kodi, wakati wa Mkutano kati yao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom, Bw. Sitho Mdlalose, baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya Waziri huyo wa Fedha na wajumbe wa Chama cha watoa Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA), jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiongoza Mkutano kati yake na wajumbe wa Chama cha watoa Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA), jijini Dodoma, ulioangazia maboresho ya Sera za Kiuchumi na Kikodi.
Mjumbe wa Chama cha watoa Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA) kutoka Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom, Bi. Hilda Bujiku, akichangia hoja wakati wa Mkutano kati yao na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), jijini Dodoma.
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Kampuni za Simu, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), alipokuwa akizungumzia vyanzo vipya vya kodi, wakati wa Mkutano wa Waziri huyo na wajumbe wa Chama cha watoa Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA), jijini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa tano kushoto), Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Mawasiliano, Mhe. Nape Nauye (wan ne kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango- Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali (wa tano kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom, Bw. Sitho Mdlalose (wa nne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi kutoka Kampuni za Simu, baada ya kumalizika kwa Mkutano katiyao, jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)
**************************
Saidina Msangi na Peter Haule, WFM-Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekihakikishia Chama cha Watoa Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA) kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara yatakayo iwezesha Sekta Binafsi kukua na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Mhe. Nchemba alisema hayo jijini Dodoma alipokutana na kuzungumza na Chama cha Watoa Huduma wa Simu Tanzania (TAMNOA), wakati kikiwasilisha Serikalini maoni yao kuhusu sera za kodi ikiwa ni maandalizi ya Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/23.
“Sekta binafsi ikinawiri na Serikali inanawiri! Kwa sababu sekta binafsi ndiyo injini ya kuwezesha ukuaji wa uchumi wetu, kwa hiyo niwashukuru kwa maoni mliyotoa yakiwemo ya kutoza kodi maeneo yenye kipato kikubwa na kutoa msamaha wa kodi kwa wale wenye kipato kidogo ili kupunguza pengo la walio nacho na wasio nacho”, alisema Dkt. Nchemba.
Dkt. Nchemba alisema kuwa dira ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kuona sekta binafsi inafanya kazi kwa mafanikio makubwa, kwa kuwa ni injini ya kukua kwa uchumi wetu, chanzo cha ajira kwa vijana lakini pia ni chanzo cha mapato kwa Serikali, hivyo ikikua na mapato ya Serikali yatakua.
Alisema kama Wizara imepokea maoni hayo na itasimamia utekelezaji wake ili kuangalia mianya mipya ya kutoza kodi hususani kampuni kubwa duniani zinazofanya biashara kwa njia ya kidijiti kwa kuweka sheria ili kodi hizo ziweze kutumika kutoa huduma kwa wananchi.
Aliwaelekeza wataalamu wa Wizara hiyo kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia mapendekezo yaliyotolewa na wadau hao ili kuona namna bora ya kuyatumia mapendekezo hayo.
Aidha, Waziri Nchemba alitoa wito kwa wadau wengine ikiwemo Sekta binafsi nchini kuwasilisha mapendekezo na maoni yao mapema kuelekea maandalizi ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ili kuwa na sera za kikodi rafiki kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya nchi.
Alisema kuwa maoni na mapendekezo kutoka sekta binafsi ni muhimu katika kusaidia maboresho ya sera za kiuchumi na sera za kikodi ili kujenga mazingira rafiki kwa sekta binafsi nchini.
Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, alisema kuwa mawazo yaliyotolewa na wadau ni mazuri na kuwa Serikali imeyachukua na yatafanyiwa kazi na kuiomba Wizara ya Fedha kuchambua maoni hayo mapema na kuwashirikisha wadau kuhusu maamuzi yatakayofikiwa.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, alisema kuwa suala la kuangalia namna ya kuzitoza kodi kampuni kubwa duniani zinazofanya biashara kwa njia ya mtandao ni muhimu kwa kuwa yanakusanya fedha nyingi kutoka kwa wananchi lakini haziachi chochote kwa ajili ya maendeleo yao.
Kwa upende wao Chama cha Watoa Huduma za Simu Tanzania (TAMNOA) walisema kuwa mapendekezo waliyoyatoa yakifanyiwa kazi na kuanza utekelezaji wake mapato ya Serikali yataongezeka kutoka asilimia 61 hadi asilimia 64.9.