Baadhi ya machinga Manispaa ya Iringa wakipaza sauti zao juu ya mgomo wao wa kutoondoka mashine tatu na miomboniBaadhi ya machinga Manispaa ya Iringa wakipaza sauti zao juu ya mgomo wao wa kutoondoka mashine tatu na miomboni.
*******************************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
WAFANYABIASHARA wadogo wadogo (MACHINGA) mkoani Iringa
wameugomea uongozi wa manispaa ya Iringa kuhama katika eneo la mashine tatu na
miomboni ambalo wanafanyia biashara zao hivi sasa.
Akizungumza na waandishi wa Habari katibu wa MACHINGA
mkoa wa Iringa Joseph Kilienyi alisema kuwa uongozi wa manispaa ya Iringa
wamewapangia eneo ambalo sio Rafiki kwa biashara ambazo wanazifanya hivyo
wameamua kugoma kuondoka katika maeneo ambayo wanafanyia biashara hivi sasa.
Alisema kuwa serikali ya manispaa ya Iringa
imewapangia wahamie katika eneo la welfare ambalo wanadai ni dogo halafu sio
Rafiki kwa baishara ambazo wanafanya kwa kuwa ni vigumu wateje kuwafikia katika
eneo hilo.
Kilienyi alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliwaangazi viongozi wa
wilaya,halmashauri na mikoa kuwapanga MACHINGA katika maeneo ambayo Rafiki kwa
biashara zao kwa kushirikiana na viongo wa wafanya biashara hao ila jambo hilo
kwa manispaa ya Iringa Limekuwa kinyume na maagizo hayo.
Alisema wataendelea kugoma hadi mwisho kuondoka katika
maeneo ya miomboni na mashine tatu hadi pale serikali ya manispaa ya Iringa
itakapo watafutia eneo Rafiki kwa biashara zao ambapo wao wanategemea sana
wateja wapita njia.
Kwa upande wake mwenyekiti wa MACHINGA mkoa wa Iringa
Yahaya Mpelembwa alisema kuwa eneo ambalo linawafa wafanyabiashara hao ni eneo
la makaburi ya Mlande ambapo kuna eneo kubwa na Rafiki kwa wafanyabiashara hao
kufanya biashara zao.
Alisema eneo pekee ambalo watakubali kwenda kufanya
biashara zao ni eneo la makaburi ya Mlandege kwa kuwa kuna eneo kubwa na Rafiki
kwa bishara zao kinyume cha hapo hawapo tayari kuhama katika maeneo yam ashine
tatu na miomboni ambyo kwa sasa ndio wanafanya shughuli zao za biashara.
Mpelembwa alisema kuwa eneo la welfare ambalo
wamepangiwa na serikali ya Manispaa ya Iringa hawawezi kwenda kwa sababu eneo
ni dogo hala halina mzunguko wa watu wengi ambao wangeweza kununua bidhaa zao.
Zeche Zabron aliyekuwa mwenyekiti wa MACHINGA mkoa wa
Iringa alisema kuwa wafanyabisha hao wanatakiwa kwenda katika makaburi ya
Mlandege tu na sio sehemu nyingine kwa kuwa makaburi hayo yanaweza kuondolewa
kwa kuwa yamekaa miaka mingi ambayo kisheria yanatakiwa kuondolewa kwa kufuata
tu utaratibu husika.
Alisema hakuna sheria inayokatakaza makaburi
kuhamishwa hivyo ameutaka uongozi wa manispaa ya Iringa kuhakikisha
wanayaoondoa makaburi hayo kwa mujibu wa sheria za nchi kama ambavyo inatakiwa
la sio watalazimika kwenye mahakani kwa hoja ya kuyaondoa makaburi hayo.
Zeche alisema kuwa uongozi wa manispaa ya Iringa
unafanya mambo ambayo wanaamua bila kuwashirkisha viongozi wao waliopo
madarakani kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan alivyowaagiza.
Akijibia kero hizo Meya wa manispaa ya Iringa Ibrahim
Ngwada alisema kuwa kila hatua wanayoifanya ya kuwahamisha MACHINGA katika
manispaa hiyo wamekuwa wakiwashirikisha viongozi wao mara kwa mara anashangaa
kuona wameanza kuyageuka majadiliano yao.
Alisema kuwa walikubaliana na viongo wa umoja huo kuwa
eneo Rafiki kwa biashara yao ni eneo la welfare na serikali ikawekeza fedha
nyingi ambazo zimetumika kujenga mabanda ya kufanyia biashara na yamekamika
sasa anashangaa kuona kumeanza maneno mengine ambayo hayana afya kwa maendeleo
ya manispaa ya Iringa.
Ngwada alisema kuwa viongozi wa MACHINGA wamekuwa
wakilitaka eneo la makaburi ya Mlandenge jambo ambalo ni gumu kufanyika
kutokana na historia ya makaburi hayo.
Alisema kuwa makaburi hayo bado hayajafikiwa muda wa
kuyaondoa kwa kuwa bado kuna makaburi ya miaka 40 toka mtu wa mwisho azikwe
pili kutakiwa kutafuta sehemu nyingine ya kuhamishia miili ya marehemu
waliozikwa katika makaburi hayo.
Ngwada alisema kuwa ili kuyaondoa makaburi hayo ni
lazima kuwashirkisha wananchi,viongozi wa dini wizara husika na kutathimini
gharama halisi ya makaburi hayo na kuingalia sheria inasema na vyote hivyo
havijafanyika na viongozi wa MACHINGA Iringa wanataka tu yaondoke wapewe eneo
hilo wafanyie biashara.
Alisema kuwa watu waliozikwa katika eneo hilo wanathimini
kwa mchango wa kimaendeleo walioufanya hadi kuifikisha manispaa ya Iringa
ilipofika hivyo sio japo jepesi kiasi hicho cha kuyaondoa makabuli hayo.
Ngwada alisema kuwa kuna maeneo mengi ambayo MACHINGA
wa Manispaa ya Iringa wanatakiwa kufanyia biashara sio eneo ambalo holo
wanalolihitaji kwa kutumia mashinikizo bila kujali wataalam wanasema nini.
Nao wazee wa Manispaa ya Iringa wamelaani kitendo cha MACHINGA
wa Iringa kutaka kuyaondoa makaburi hayo kwa kuwa hawajui historia ya makaburi
hayo na mchango ulifanywa na watu waliozikwa kwenye makaburi hayo ya Mlandege.
Walisema kuwa asilimia kubwa ya wananchi waliokuwa
wanapigania maendeleo ya mkoa wa Iringa walizikwa pale ilikuwa kwa kunyongwa na
wakoloni kutokana na kutafuta uhuru na kuleta maendeleo ya Iringa.
Waliwataka viongozi wa machinga Iringa kukaa pamoja na
serikali ya manispaa ya Iringa na kutafuta eneo linguine la kufanyia biashara
hizo kwa kuwa bado kuna maeneo mengi yapo wazi kwa ajili ya biashara zao.
Wazee hao walitoa ovyo kwa mtu yeyote yule atakae
husika kuyaondoa makaburi hayo kwa maslai yake binafsi atapata laana kutoka kwa
mashujaa hao ambao wamezikwa hapo.