…………………………………………………..
Mwamvua Mwinyi Pwani
Halmashauri ya Mji Kibaha ,hadi kufikia 28 Januari,2022 imeshapokea jumla ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza 3,647 kati ya 4,611 waliochaguliwa ambayo ni sawa na Asilimia 79.
Akitoa taarifa hiyo,Kaimu Afisa Elimu Sekondari ,Zena Mkopi alisema jumla ya waliochaguliwa wavulana ni 2,364 na wasichana ni 2,247 wanaofanya jumla yao kuwa 4,611.
Aidha ambao wamesharipoti kwenye shule zote 16 ni 3,647 wavulana wakiwa 1,843 na wasichana 1,804 sawa na 79 asilimia.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha ,Mhandisi Mshamu Munde alisema kuwa Wanafunzi wote wanasoma kwenye Mazingira rafiki kwani miundombinu yote ipo vizuri huku akitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha Milioni 940 zilizojenga Madarasa 47 kuondoa kero ya uhaba wa Madarasa
Rashid Abdallah kwa niaba ya Wanafunzi alisema kuwa hawana la kumlipa Rais Samia lakini wanaahidi kusoma kwa bidiii kama fadhila kwake na Serikali anayoiongoza.
Pia kati ya Madarasa 47 yaliyojengwa kwa fedha za Mapambano dhidi ya Uviko-19 kiasi cha milioni 940, Madawati 1365 pia yametengenezwa.