**************************
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetangaza kuongeza muda wa utoaji Elimu na Huduma katika eneo la Mlimani City Jijini Dar es Salaam hadi siku ya jumatano Februari 2, 2022.
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano BRELA inasema kuwa hatua hiyo imetokana na wadau wengi kujitokeza kwa wingi kupata Huduma mbalimbali zinazotolewa na BRELA katika muda wa siku tano zilizopangwa awali hivyo kulazimu kuongeza muda wa siku tatu ili kuendelea kutoa Huduma kwa ufanisi zaidi.
BRELA inawahimiza wananchi kufika katika viwanja vya Mlimani City ili kupata Elimu na Huduma mbalimbali inazotoa.