Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirikika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Nchini, Mahoua Bamba Parums, kuhusu masuala mbalimbali ya wakimbizi, katika Kikao kilichofanyika Ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimsindikiza Mwakilishi Mkazi wa Shirikika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Nchini, Mahoua Bamba Parums, baada ya kumaliza mazungumzo yao kuhusu masuala mbalimbali ya wakimbizi, katika Kikao kilichofanyika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma kwa Wakimbizi, Sudi Mwakibasi, alipokuwa anamfafanulia jambo kabla ya kikao cha Waziri huyo na Mwakilishi Mkazi wa Shirikika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Nchini, Mahoua Bamba Parums, kuhusu masuala mbalimbali ya wakimbizi. Kikao hicho kilifanyika Ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Shirikika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Nchini, Mahoua Bamba Parums, wakati Mwakalishi huyo alipokuwa anawasili ofisini kwa Waziri kujadiliana masuala mbalimbali ya wakimbizi, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
**********************
Na WMNN, Dar es Salaam.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Shirikika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini kufanya kazi kwa kuzingatia sera, sheria na vipaumbele vya Serikali katika utendaji wake.
Masauni amezungumza hayo jijini Dar es Salaam, leo, katika Kikao na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirikika hilo Nchini, Mahoua Bamba Parums, ambaye alifika ofisini kwa Waziri huyo kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuwasili nchini mwishoni mwa mwaka jana.
“Karibu sana Tanzania na pia nakupongeza sana kwa kuteuliwa katika nafasi hii, natumai kupitia Shirika lako hapa nchini tutafanya kazi vizuri kwa kuzingatia sera, sheria na vipaumbele vya serikali katika utendaji wako,” alisema Masauni.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi huyo, Mahoua, pia alimpongeza Waziri huyo kwa kuteuliwa kwenye nafasi hiyo kuiongoza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
“Nakupongeza Mheshimiwa Waziri kwa kuteuliwa kwa kuteuliwa kuwa Waziri na pia naipongeza Tanzania kwa ukarimu wake wa kuendelea kupokea na kuhifadhi wakimbizi kwa miaka mingi sasa na naomba muendelee kufanya hivyo,” alisema Mahoua.
Pia Mwakilishi Mkazi huyo alimuhakikishia Waziri kuendeleza ushirikiano katika shughuli za hifadhi ya wakimbizi na UNHCR itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuwahudumia Wakimbizi.