Dk. Shein akiwasili katika Viwanja Vya Mwehe, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, katika sherehe za ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.
Dk. Shein akivalishwa skafu baada ya kuwasili katika Viwanja Vya Mwehe, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja, katika sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.
Viongozi mbalimbali wakimlaki Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alipowasili katika viwanja vya Mwehe, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika tukio la Ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM iliyofanyika katika viwanja vya Mwehe, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Vijana wa halaiki wakitumbuiza kwa nyimbo na kuandika mambo mbalimbali wakati wa sherehe za Ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Zanzibar), Dkt. Ali Mohamed Shein,akizungumza wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwehe Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, akizungumza kuwasilisha salamu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Katika sherehe za Ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM iliyofanyika katika viwanja vya Mwehe Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwasilisha salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT), katika sherehe za Ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwehe Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo,,akizungumza wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwehe Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka,akizungumza wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwehe Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
(PICHA ZOTE NA CCM MAKAO MAKUU)
………………………………………………….
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimezindua wiki ya maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM katika sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Mwehe Makunduchi, Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, aliwataka watendaji katika Chama na serikali kwenda na kasi ya mabadiliko ili kufanikisha tija na maendeleo ya nchi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Daniel Chongolo, akizungumza katika uzinduzi huo alisema katika miaka 45 iliyopita CCM imezidi kuwa imara ikiwamo kuhimili ushindani ndani ya mfumo wa vyama na kwamba inaendelea kwenda na kasi ili kuleta maendeleo zaidi.
Kauli mbiu ya sherehe hizo ni CHAMA IMARA SHIRIKI UCHAGUZI KWA UADILIFU
Chongolo alisema pia siku ya kilele cha sherehe hizo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi atazindua kadi za uanachama za kielekroniki.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdallah, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, wabunge, wawakilishi, viongozi wa serikali na wananchi.