Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na ujumbe alioambatana nao kutoka Tanzania akimsikiliza Kiongozi wa Vyama vya Wasafirishaji Watalii wa nchini Marekani, Rumit Mehta katika ofisi za Ubalozi za Tanzania katika ofisi za New York za nchini Marekani ambapo Waziri Ndumbaro pamoja na mengine ameamulika Kiongozi huyo kuja Tanzania kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko ukanda wa Kusini.Wengine ni watumishi wa Ubalozi Tanzania nchini Marekani katika ofisi za New York
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na ujumbe alioambatana nao kutoka Tanzania akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania katika ofisi za New York za nchini Marekani mara baada ya kikao kilichofanyika baina yao ambapo ametoa wito kwa Watumishi hao kutekeleza Diplomasia ya Uchumi ipasavyo, Wa nne kulia ni kiongozi Vyama vya wa Wasafirishaji Watalii wa nchini Marekani, Rumit Mehta
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na Mjumbe wa Bodi ya Misitu Tanzania, Lilian Ngwanakilila akimsikiliza Kiongozi wa Vyama vya Wasafirishaji Watalii wa nchini Marekani, Rumit Mehta katika ofisi za Ubalozi za Tanzania za New York nchini Marekani ambapo Waziri Ndumbaro pamoja na mengine ameamulika Kiongozi huyo kuja Tanzania kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko ukanda wa Kusini
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa kwenye picha pamoja na Kiongozi wa Vyama vya Wasafirishaji Watalii wa nchini Marekani, Rumit Mehta wakiwa wameshika picha ya twiga katika ofisi za Ubalozi za Tanzania nchini Marekani katika ofis za New York mara baada ya kumaliza kikao kilicholenga kuimarisha ushirikiano kwenye sekta ya utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa nakiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania katika ofisi za New York za nchini Marekani mara baada ya kikao kilichofanyika baina yao ambapo ametoa wito kwa Watumishi hao kutekeleza Diplomasia ya Uchumi ipasavyo, Wa nne kulia ni kiongozi Vyama vya wa Wasafirishaji Watalii w nchini Marekani, Rumit Mehta
…………………………………………………………….
NA MWANDISHI MAALUM, NEW YORK, MAREKANI
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amewataka Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kuweka nguvu za kutosha katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi ikiwemo kuwavutia watalii kutoka nje ya nchi kuja nchini.
Ametoa kauli hiyo leo wakati mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea ofisi ya Ubalozi huo ikiwa ni muendelezo wa kuzungumza na Watumishi na Wawekezaji mara baada ya kumalizika kufanyika kwa mkutano wa 50 wa mwaka wa uwindaji wa kitalii uliofanyika katika Jiji la Las Vegas nchini Mareakani.
Akizungumza na timu ya Watumishi hao, Dkt. Ndumbaro amempongeza Balozi wa Tanzania Nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza kwa kazi kubwa anayoifanya ya Diplomasia katika tasnia ya biashara na utalii.
” Nimevutiwa mno kwa jinsi unavyoitendea haki Diplomasia ya uchumi natamani Mabalozi wwngine wanaioziwakilisha nchi zetu nchi za nje wajifunze kutoka kwako” amesisitiza Dkt.Ndumbaro
Ambapo amewataka Wanadiplomasia hao kuwa daraja katika kuwawezesha watalii kuja nchini Tanzania
Dkt.Ndumbaro amesema Diplomasia ya uchumi katika tasnia ya utalii inapaswa kutangaza na kujibu maswali ya watu mbalimbali wanaotaka kutalii Tanzania kuhusu namna ya kufika nchini kiujumla na katika kila kivutio cha utalii kimahususi.
“Kutokana na kasi kubwa ya maendeleo ya kiuchumi, Mabalozi wanaoziwakilisha nchi Diplomasia ya kiuchumi ndo injini ya maendeleo haikwepi, ongezeni ujuzi katika eneo hili.” amesisitiza Dkt. Ndumbaro.
Aidha, Dkt. Ndumbaro amewahimiza Watumishi hao kuwa mstari wa mbele katika kujua masuala ya uwekezaji na biashara pamoja na mambo yote muhimu kuhusu utalii nchini ili waweze kuwaelezea wananchi wanaowahudumia
Vilevile amewataka Wanadiplomasia hao kuwa kichocheo cha watalii kutoka katika nchi waliyopo kuhudhuria katika mikutano, makongamano na maonyesho ya utalii ya ndani ya Tanzania ikiwemo
matamasha ya kiutamaduni .
Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro amemwalika nchini Tanzania, Kiongozi wa Vyama vya Waongoza Watalii nchini Marekani, Rumit Mehta kuja kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko Ukanda wa Kusini